Sina uzoefu na OUT na sijui curriculum yao ila Data Science ni kozi nzuri ajira zipo. Ulimwengu umebadilika we have loads of data ila hakuna analysts.
Data scientists wanafanya kazi mahali popote pale zilipo takwimu. Kwa Tanzania, fursa za ajira serikalini sio nyingi sana inabidi ujiongeze na ufanye networking hapo utaweza kujiajiri.
Darasani utasoma statistics na programming languages kama Python na Pascal. Kama utasoma OUT, enroll for online courses za edX zitasupplement vitu vingi ambavyo sidhani kama utacover ukiwa OUT.
Ni vizuri ukasoma Data Science na specialisation nyingine mfano ukifanya Economics au Finance na Data Science unakuwa Financial Analyst. Ukifanya hivi unaongezea uelewa wa mambo na chances za kuajiriwa ama kujiajiri kama mshauri au mtafiti.
Analysts wengi field hawasomi BSc Data Science undergraduate; wengi wana degrees in different fields kama Accounting, Finance, Statistics, Econ ama Public Health. Vitu vingi unajifunza on job!
Kila la heri.