Bachelors Club: Tuzungumze

Bachelors Club: Tuzungumze

Kama nilivyosema wakati najaribu kuchangia mada kuhusu sababu za kuvunja ndoa, mapungufu mengi yanazungumzika na yanarekebishika. Kwa hiyo njia kubwa ni kukaa chini na kuelezana mapungufu yetu kwa nia ya kurekebishana. Hapa sasa cha kuangalia ni approach na lugha utakayotumia. Nadhani huwa unasikia hapa jamvini watu wanashauri kwamba 'mtoa out halafu ukazungumze naye kwa upole uko'. Hii ni approach ambayo wengi tunaitumia, and normaly it works (of course depending on the issue itself). Katika mazungumzo yenu mnaweza kuwa wenyewe tu au mkahusisha ndg, jamaa na marafiki especially kama mmeshindwa kufikia muafaka nyie wenyewe.
mito Kwanza pongezi kwa kwenda kanisani ..........hebu tuendelee, nimeipenda hiyo approach yako na kama nilikuelewa mwanzo ni kwamba kosa lisilosameheka kwako ni cheating.............lakini hebu angalia umeweka msingi mzuri sana wa namna ya kutatua changamoto ndani kwa nini usi-include na cheating kama changamoto inayotatulika (angalau likiwa kosa la kwanza)...............

Kwa sababu pengine anaweza ku-cheat kwa sababu ambayo inaweza kuelezeka (ulikuwa masomoni kwa miaka 3 nje ya nchi, ofisini kwake kuna vjana mabarubaru na kama ujuavyo tamaa wakati mwingine huwaka mwilini shetani akampitia na akaanguka dhambini) ni kosa amefanya but anakiri na kuomba msamaha......haiwezekani ukamsamehe?

Lakini hebu tuone makosa mengine ambayo kwangu mimi ni makubwa zaidi (kwako cheating ndilo baya sana na lisilosameheka)....................Mmeoana na mko kwenye ndoa takribani miaka 5 halafu unakuja kugundua kwamba ana mtoto aliyemzaa kabla hamjaoana na hakuwahi kukwambia.............Hivi na hili kwako linasameheka? (kama ndio/hapana kwa nini?
 
Last edited by a moderator:
Evidence ya cheating ni ngumu sana.........ni rahisi kwa mfano wewe mke wako kupata ushahidi wa cheating kuliko wewe ambavyo unaweza kumkamata.............Unaweza kutumia ushahidi wa mazingira kumwacha mkeo? Au utasubiri kwa maumivu makali ushahidi wa papo kwa papo?

Hebu tuseme ndio imetokea huta-consider factors nyingine kabla ya kuamua? (kama watoto, namna wewe na mkeo mlivyoanza maisha mkiwa hamna na senti na leo baada ya miaka 10 au 20 kosa moja linafuta historia yote nzuri?)

platozoom cheating ninayomaanisha mimi ni ile ambayo mimi mwenyewe nimejiridhisha bila chenga (confirmed). Siwezi kufanya uamuzi based on hearsay evidence. Najua ni kwali hearsay evidence tu zitakufanya usikie maumivu makali moyoni mwako. Hapa sasa ndo inabidi uonyeshe uvumilivu wako kama mwanaume. Unajua mimi kama mimi huwa napenda nikitoa uamuzi fulani basi uamuzi huo uonekane sahihi hata mbele za ndg, jamaa na marafiki zangu. Hivyo huwa napenda kuvuta subira ili nijiridhishe kwanza, isije ikaonekana nimemuonea mwenzi wangu. So hadi nitakapo-prove hizo hearsay ndo nitaamini.

Halafu siku zote ninaamini palipo na ukweli always uongo unajitenga, zaidi ya yote naamini kuwa za mwizi ni arobaini. Hivyo ataficha lakini naamini ipo siku nitajua tu.

Ni kweli hizo factors ulizo-mention ni muhimu mno kuweza kufuta historia nzuri ya maisha yenu. Shida yangu kama nilivyosema kuhusu cheating ni kwamba najiona sitaweza kumwamini na kumpenda tena kama ilivyokuwa awali. Kifupi nita-pretend tu kumsamehe pengine kwa kuzingatia factors ulizo-mention, ila sitaishi naye kwa amani tena, nitaishi naye kifeki feki tu! Kumbuka hapa najiongelea mimi kama mimi, pengine labda ni kwa sababu mimi mwenyewe si-cheat ndo maana nakuwa na feeling za namna hii!
 
unaikumbuka ahadi yetu?five years from last year
tukutane hapa jf au popote nikuulize kuhusu
ndoa na misimamo yako ya sasa....
usisahau....

Naona kuna kitu interesting hapo kati yako na nyumba kubwa.......unaweza kukumbushia kidogo tupanue mjadala!
 
Last edited by a moderator:
Mjadala mzuri sana. Ila naomba nitachangia kesho leo ni siku ya kuienzi familia au wanasema family time. Jambo pekee la kufanya leo ni kukaa na familia. Kusikia mashtaka ya watoto na kutatua miggoro yao ya wiki nzima na kujaribu kusuluhisha pale ulipogombana na mama wiki hii.
 
Wewe The Boss mimi si mwanadoa mpya...Nafukuzia miaka kumi...huu ni mwaka wa 8 plus. Na nimeanza kutoka na jamaa 12 years a go (4 years before marriage)

Sasa miaka mitano (minne) baadae itakuwa na impact gani kwangu? Sana sana nategemea ndoa kuwa tamu mara mbili kwani watoto wanazidi kukua na kutupa nafasi ya kutanua kama tulipokuwa wawili.

unaikumbuka ahadi yetu?five years from last year
tukutane hapa jf au popote nikuulize kuhusu
ndoa na misimamo yako ya sasa....
usisahau....
 
Watoto hawafanyi challenges kuwa ngumu ila wanapunguza uzito wa challenge. Mi jamaa akiniboa ninakuwa na sababu ya kuendelea kumvumilia kwa kuwa nimezungukwa na vijana wanaonipenda (wanangu) ambao siwezi kuwatoa kwa baba yao na baba yao hawezi kuwatenga nami. Watoto ni sababu inayofanya kusamehe kuwe possible kwenye ndoa.

Hivyo siwezi kuwa na stress kihivyoooo...nina wafariji wangu (my sons) ambao wanafanya nitabasamu muda wote na hiyo tabasamu nadhani inamfanya jamaa nae hata kama tumenuniana arudishe majeshi.

Sawa watoto wanapunguza challenge lakini kulikoni hao wenye watoto wanashindwa ku-handle hizo challenge?
 
Wewe The Boss mimi si mwanadoa mpya...Nafukuzia miaka kumi...huu ni mwaka wa 8 plus. Na nimeanza kutoka na jamaa 12 years a go (4 years before marriage)

Sasa miaka mitano (minne) baadae itakuwa na impact gani kwangu? Sana sana nategemea ndoa kuwa tamu mara mbili kwani watoto wanazidi kukua na kutupa nafasi ya kutanua kama tulipokuwa wawili.

kwa hiyo for 12 years hukuwahi kuonja outside?
 
Do I need to answer that? Sidhani kwani hata nikikujibu unaweza ukaamini au usiamini... Ila wanawake wenzangu watanielewa...najua wanajua huwezi ku cheat wakati una mume unayempenda tena rijali, unacheat kutafuta nini? Pesa? Kama ni pesa wengine tuko financially independent na hatuna tamaa ya vitu vilivyo nje ya uwezo wetu?

Sikatai kuwa wanawake wana cheat...ila kuna wengi sana ambao ni waaminifu...kwani mapenzi si siri, cheater anajulikana tu.

kwa hiyo for 12 years hukuwahi kuonja outside?
 
mito Kwanza pongezi kwa kwenda kanisani ..........hebu tuendelee, nimeipenda hiyo approach yako na kama nilikuelewa mwanzo ni kwamba kosa lisilosameheka kwako ni cheating.............lakini hebu angalia umeweka msingi mzuri sana wa namna ya kutatua changamoto ndani kwa nini usi-include na cheating kama changamoto inayotatulika (angalau likiwa kosa la kwanza)...............

Kwa sababu pengine anaweza ku-cheat kwa sababu ambayo inaweza kuelezeka (ulikuwa masomoni kwa miaka 3 nje ya nchi, ofisini kwake kuna vjana mabarubaru na kama ujuavyo tamaa wakati mwingine huwaka mwilini shetani akampitia na akaanguka dhambini) ni kosa amefanya but anakiri na kuomba msamaha......haiwezekani ukamsamehe?

Lakini hebu tuone makosa mengine ambayo kwangu mimi ni makubwa zaidi (kwako cheating ndilo baya sana na lisilosameheka)....................Mmeoana na mko kwenye ndoa takribani miaka 5 halafu unakuja kugundua kwamba ana mtoto aliyemzaa kabla hamjaoana na hakuwahi kukwambia.............Hivi na hili kwako linasameheka? (kama ndio/hapana kwa nini?

Nadhani kwenye comment yangu niliyopost sasa hivi hapo juu nimeeleza kwa nini nashindwa kusamehe cheating, hivyo naomba nisijibu hapa unless more clarification is needed.

Ila hapo kwa blue: binafsi sababu za ku-cheat huwa sizikubali na zaidi huwa naziona kama ni za kutaka kuhalalisha cheating. Isitoshe huwa najitahidi sana kujenga mazingira ambayo hayatamwingiza kwenye majaribu mke wangu. Kwa mfano siwezi kukaa mbali na mke wangu kwa zaidi ya mwaka 1, huo ni utaratibu nilishajiwekea na ninaufuata. Kwahiyo hata kama niko masomoni nje ya nchi kwa muda wa miaka 3 kama ulivyosema, lazima mimi nirudi home at least once ina a year au yeye anifuate mimi niliko, at any cost. Ktk hili huwa siangalii pesa kwani kwangu mimi pesa ni second after my family.

Na kama nimepata nafasi ya masomo nje ya nchi halafu nikapiga mahesabu nikaona hakuta kuwa na nauli ya kuniwezesha mimi kwenda kwa mke wangu au yeye kuja angalau mara moja kwa mwaka, basi sitakubali hiyo nafasi. Nasema hili kwa sababu nilishagakataa nafasi mbili za kusoma nje kwa sababu ya hili.

Isitoshe familia yangu nimeijenga ktk misingi ya dini. Hivyo cheating siyo tu itavunga ndoa yetu, bali pia ni dhambi kwa Mungu. Kwa hiyo utaona hata vishawishi vya maofisini, majirani, marafiki, vijana mabarubaru n.k ni rahisi kuvishinda. Kwahiyo suala la shetani kanipitia siyo excuse hata kidogo unless uniambie umeachana na imani ya dini.
 
Ukiona watu wana watoto wanaachana baada ya miaka mitano basi jua wangekuwa hawana wangeachana ndani ya mwaka.

Nimejikuta nacheka mwenyewe...............But mwanzoni ulishauri ni vyema kukubali kuziface challeges na nafikiri hii ni step ya kwanza kwenye ndoa..............Lakini kwa kuzingatia complications kibao kwenye hiyo taasis lazima (lkama nipo sahihi) iwepo mechanism fulani ya kutatua matatizo yanayojitokeza na yatakayojitokeza bdala ya kutegemea watoto kutuliza munkari.

Au tunaishi kwa mazoea kwamba litakalotokea utatuzi utapatikana hapohapo?
Je? kila mtu ndani ya ndani anatakiwa kuwa na namna ya kukabiliana na chngamoto zinapokuja au nyote mnakuwa na namna yenu ya kutatua

Mwisho........ hivi kuna rules kwenye ndoa na nani anaziweka
 
Mjadala mzuri sana. Ila naomba nitachangia kesho leo ni siku ya kuienzi familia au wanasema family time. Jambo pekee la kufanya leo ni kukaa na familia. Kusikia mashtaka ya watoto na kutatua miggoro yao ya wiki nzima na kujaribu kusuluhisha pale ulipogombana na mama wiki hii.

Kifupi leo unafanya kazi kama ya Bernard Membe Au? Vipi una kiboko pembeni!!!!!!!!
 
Changamoto zinakabilika kama ndoa ilitokana na upendo...kama ulioa au kuolewa na right person.

Siwezi sema kwa upande wa wanaume ila kuna mabinti naweza sema ni wajinga au sijuhi nisemeje...mtu anaolewa na mwanaume huku anakua kabisa ni cha wote...afu na yeye anakuja kulalamika kuhusu matatizo ya ndoa wakati alifanya uzembe kwenye kuchagua. Mwanaume alozoea kubadili K hawezi kutulia ndani baada ya kuoa unless mtu ategemee miracles.

Kuna rafiki yangu kila siku analia na ndoa yake...ila watu siyo siri wanamcheka kwa sababu mumewe si kwamba kabadilika ila alikuwa hivyo na wamekuwa marafiki muda mrefu anamjua nje ndani. Maisha ni kupanga na kuchagua...si kukubali kila anaye propose...muangalie life after marriage. Ndoa haibadili tabia ya mtu.

Nimejikuta nacheka mwenyewe...............But mwanzoni ulishauri ni vyema kukubali kuziface challeges na nafikiri hii ni step ya kwanza kwenye ndoa..............Lakini kwa kuzingatia complications kibao kwenye hiyo taasis lazima (lkama nipo sahihi) iwepo mechanism fulani ya kutatua matatizo yanayojitokeza na yatakayojitokeza bdala ya kutegemea watoto kutuliza munkari.

Au tunaishi kwa mazoea kwamba litakalotokea utatuzi utapatikana hapohapo?
Je? kila mtu ndani ya ndani anatakiwa kuwa na namna ya kukabiliana na chngamoto zinapokuja au nyote mnakuwa na namna yenu ya kutatua

Mwisho........ hivi kuna rules kwenye ndoa na nani anaziweka
 
Nilisoma mahali watu walikuwa wanachangia Yahoo baada ya mmoja kati ya ma superstar kutangaza divorce...moja ya michango mpaka leo naukumbuka...jamaa alisema ndoa za sasa hazidumu kama zamani kwa kuwa baba na mama zetu, babu na bibi zetu walikuwa wana 'collect brocken pieces'...sisi wa kizazi hiki tuna 'throw them away'.

Najua wanaume wengi wanasema kuna kosa ambalo hawawezi samehe, nalo ni uzinzi. Lakini leo hii 90% ya wanawake either walisamehe au wana propensity to forgive cheaters. Nadhani ni sababu ya mfumo dume na ego ya wanaume..kwani kwa nchi za wenzetu wapo wanaume wanaosamehe hilo kosa. Na kama wewe unasamehewa kwa kosa hilo hilo ni kwa nini usisamehe?

Anyway point ni kuwa ndoa ni challenge kwani mmekutana ukubwani lazima kuna lots of differences. Hao ndugu wa tumbo moja tu tuna differ sana sembuse mtu kakulia na kulelewa familia nyingine.

Badala ya nyie mabachelor kukimbia challenges..nawashauri muwe na moyo wa kuzi face...ni kitu kizuri kuwa risk taker na mtu unayependa challenge...kwani hata kwenye usingo cheating zipo...brocken hearts za kumwaga...sioni mnakimbia nini. At least marriage ni commitment unaweza ku claim ownership ya ulonaye. Lol. kwa hiyo kwangu naona kuna less challenges na less risks kulinganisha na u single.

nyumba kubwa wanaume wengi huwachukulia wanawake kama mali zao, ambazo ni wao tu wanaotakiwa kuzimiliki kwa namna fulani. Mali yako ni mali yako, ikitumiwa na mtu mwingine, huumiza hisia. Lakini, mali hii inayoitwa mwanamke, mbona ina utambuzi wake? Kila wakati ukisoma kuhusu mauaji ya wivu wa kimapenzi, wanawake ndio ambao wanauawa zaidi. Lakini ukija kusoma takwimu za wanaotoka nje, wanaume ndio wanaotoka kwa kiwango cha juu sana. Kama ni kuuawa, bila shaka wanawake wangekuwa wanawaua wanaume kila siku. Hata ukiangalia kwenye fumanizi nyingi, utashangaa kuona nguvu inapelekwa kwa wanawake, badala ya wote waliofumaniwa.

naonekana kama anayefumaniwa ni mwanamke, yeye ndiye ambaye ametia aibu, na huonekana kama kahaba. Mwanaume ni mara chache sana kukumbana na misukosuko ya fumanizi, hasa kutoka kwa jamii, kwa sababu huonekana kijogoo.

Kwa nini unadhani hali iko hivyo, wakati mwanaume ndiye mtokaji nje mzuri?

Ni kwa sababu wanaume hujawa na wivu zaidi pale suala linapohusu mwili kuliko hisia. Wataalamu wanasema, mwanaume anapofikiria kuhusu kumfumania mke au mpenzi wake, picha zinazoenda kwenye mawazo yake ni zile zenye kuhusu mwili. Atatengeneza picha za mkewe au mpenzi wake na huyo mwanaume wakiwa pamoja kwenye tendo. Ataona kila kitu ambacho hufanya na mkewe kikiwa kinafanywa na mtu huyo na pengine ataona ziada. Lakini, picha zote zitakuwa zinahusu shughuli za kimwili.

Lakini kwa mwanamke picha zitakuwa ni za mwili, lakini pia za kujali. Mwanamke atafikiria au kujenga picha kwamba, mumewe au mpenzi wake ameenda shopping na huyo hawara na anamnunulia vitu vya thamani. Halafu atajenga picha wakiwa pamoja wakiwa wanazungmza kwa furaha na bashasha. Mwanamke huona wivu kimwili na hisia. Tafiti zinaonesha kwamba, vipigo na vifo vingi dhidi ya wanawake kutoka kwa wapenzi wao hutokana na wivu. Kwa hali hiyo, wivu unaongoza katika kusababisha maumivu ya kimwili na hisia kwa wanawake, na pengine hata kifo………………...
 
Tunakabili vipi hizo changamoto "mwanaume kidume v/s mwanamke kidume au mnyonge
 
platozoom hakuna cha kiboko wala nini. Ni maneno tuu ya busara yanatosha aise. Kiboko kimepitwa na wakati bana.

Sawa........utakapomaliza kusluhisha kesi uzoefu wako unahitajika hapa kwenye "bachelor club" yetu. Karibu
 
Wewe The Boss mimi si mwanadoa mpya...Nafukuzia miaka kumi...huu ni mwaka wa 8 plus. Na nimeanza kutoka na jamaa 12 years a go (4 years before marriage)

Sasa miaka mitano (minne) baadae itakuwa na impact gani kwangu? Sana sana nategemea ndoa kuwa tamu mara mbili kwani watoto wanazidi kukua na kutupa nafasi ya kutanua kama tulipokuwa wawili.
nyumba kubwa hapo kwenye bold kumbe mimi na wewe ngoma droo eh.............!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom