platozoom
JF-Expert Member
- Jan 24, 2012
- 9,424
- 11,320
- Thread starter
-
- #41
mito Kwanza pongezi kwa kwenda kanisani ..........hebu tuendelee, nimeipenda hiyo approach yako na kama nilikuelewa mwanzo ni kwamba kosa lisilosameheka kwako ni cheating.............lakini hebu angalia umeweka msingi mzuri sana wa namna ya kutatua changamoto ndani kwa nini usi-include na cheating kama changamoto inayotatulika (angalau likiwa kosa la kwanza)...............Kama nilivyosema wakati najaribu kuchangia mada kuhusu sababu za kuvunja ndoa, mapungufu mengi yanazungumzika na yanarekebishika. Kwa hiyo njia kubwa ni kukaa chini na kuelezana mapungufu yetu kwa nia ya kurekebishana. Hapa sasa cha kuangalia ni approach na lugha utakayotumia. Nadhani huwa unasikia hapa jamvini watu wanashauri kwamba 'mtoa out halafu ukazungumze naye kwa upole uko'. Hii ni approach ambayo wengi tunaitumia, and normaly it works (of course depending on the issue itself). Katika mazungumzo yenu mnaweza kuwa wenyewe tu au mkahusisha ndg, jamaa na marafiki especially kama mmeshindwa kufikia muafaka nyie wenyewe.
Kwa sababu pengine anaweza ku-cheat kwa sababu ambayo inaweza kuelezeka (ulikuwa masomoni kwa miaka 3 nje ya nchi, ofisini kwake kuna vjana mabarubaru na kama ujuavyo tamaa wakati mwingine huwaka mwilini shetani akampitia na akaanguka dhambini) ni kosa amefanya but anakiri na kuomba msamaha......haiwezekani ukamsamehe?
Lakini hebu tuone makosa mengine ambayo kwangu mimi ni makubwa zaidi (kwako cheating ndilo baya sana na lisilosameheka)....................Mmeoana na mko kwenye ndoa takribani miaka 5 halafu unakuja kugundua kwamba ana mtoto aliyemzaa kabla hamjaoana na hakuwahi kukwambia.............Hivi na hili kwako linasameheka? (kama ndio/hapana kwa nini?
Last edited by a moderator: