Bachelors Club: Tuzungumze

Asante kwa kutukumbusha hilo Mtambuzi.

Mwanamke ni mwanamke na mwanaume ni mwanaume...haya mambo ya usawa ni kupingana na nature. Lol.


 
Nimekumbuka siri nyingine ya ndoa. Hakuna mwanaume anapenda kudhalilishwa uanaume wake, au niseme u kichwa wake wa familia adharani.



Mimi wakati mwingine nakuwa mkorofi lakini sijawahi kufanya ukorofi wangu kukiwa na third person. Nazingatia sana heshima kwa mume wangu mbele za watu including kuchagua cha kuongea.

Najua kuna mtakaosema kwa nini na pretend nikiona watu...lakini nawahakikishia ina work...mume wangu anaheshimiwa kwa kuwa mimi naonekana niko chini yake at least machoni pa jamii. Lol.
 
Asante kwa kutukumbusha hilo Mtambuzi.

Mwanamke ni mwanamke na mwanaume ni mwanaume...haya mambo ya usawa ni kupingana na nature. Lol.

Sikutegemea statement kama hii kutoka kwako.........may be kwa sababu avatar pengine imenidanganya. Bravo!!
 

Correct
 
nyumba kubwa hebu subiri kwanza, hivi wewe sio dada yake Mama Ngina Kweli......?
Isije ikawa namkosea adabu shemeji yangu wakati mwingine humu jamvini......................! Vijitabia vyako unavyovizungumzia humu jamvini, Mama Ngina mtupu na dada yake yuko hivyo hivyo..................................LOL
 
Last edited by a moderator:

Mmmmmmmmm isje ikawa maneno ya kiutu-uzima
 
Mkuu platozoom japo wengine hujatuita any wayz ngoja tujikaribishe ili tuchangie mada tajwa hapo chini...Nidiklee interest kuwa mimi nilishwahi kuwa na ndoa but currently i am a senior bachelor

1. Kwa nini watu wanaoa/kwa nini tuoe?
Kuoa au kuolewa nadhani kimantiki zaidi hili ni suala la kijamii yaan ni lazima tuwe na familia ili kuendeleza kizazi. Lakini ili udumu kwenye NDOA hapa inatakiwa tuheshimu zaidi HISIA..Mfano ni rahisi wanadamu kukushauri kuhusu Ndoa kiujumla ..but inakuwa ngumu kukushauri namna ya kuishi na mwenzi wako kila siku..kama walivyosema wengine..muungano wa watu wawili waliokutana UKUBWANI unataka mshibane HISIA na KUVUMILIANA..na haya mambo mara nyingi sio rahisi kuyajua kabla haujaingia na kumbuka kila ndoa ni 'unique'..Ushauri: Unapoingia kwenye ndoa jiweke kwenye nafasi ya kusuluhisha kuliko kulaumu!

2. Changamoto za kuzingatia kwenye ndoa
Changamoto kubwa ninayoiona kwenye NDOA ni kuhusu namna yenyewe ya kuishi yaan 'Jinsi ya kutafuta fedha na kupanga maisha kwa fedha iliyopo'..Ikumbukwe shina KUU la maovu ni pesa..hivyo kama mtajitahidi kufanana misimamo kwenye namna ya kuishi na mipango ya maendeleo kwa ujumla..mingi ya migogoro itapungua..sisemi haitakuwepo!

3. Sababu zipi za zitakufanya uvunje ndoa
Kwangu mie sababu kubwa ya kuvunja ndoa ni DHARAU ikiingia..Itoshe kusema kuwa 'cheating' ni zao la dharau..so, kama kuna mazingira ya Kudharauriana kwenye NDOA ..obvious ndoa hiyo kwa mujibu wangu mie haitofika mbali..
 
Last edited by a moderator:
Mkuu snowball@ huu ni mjadala wa wazi, hao niliowaita walikuwa "main speakers" lakini hatimaye kila mtu anaruhusiwa kuchangia...........lengo likiwa kupata majibu mujarab na kuzifahamu changamoto za ndani ili tupate picha nini kinatakiwa kufanyika.

Anyway hapa kwako nimepata kitu kingine "dharau'. Nakumbuka mito aliisema hii lakini pia wewe umeenda mbali zaidi na kusema cheating ni zao la dharau. Nakumbuka nyumba kubwa naye kasema pia ukichagua the right person si rahisi kupata hiyo changamoto, kwa maana kwamba huwezi kumchagua mtu ambaye unajua kabisa player hatari ukitegemea akiingia kwenye ndoa atabadilika.

Kwanza pole kwa kupoteza ndoa yako........ but kwa mtazamo wako main reason ya hizo dharau ni ipi na kwa vipi ulishindwa kukabiliana nayo au haina suluhisho?

Na kwa kuongezea hapa ulisema hivi " mtajitahidi kufanana misimamo kwenye namna ya kuishi na mipango ya maendeleo kwa ujumla..mingi ya migogoro itapungua..sisemi haitakuwepo!".............Sasa hapa umegundua kwa hakika misimamo yenu ipo tofauti sana kuhusu hilo................suluhisho ni kuachana?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu @platozoom unajua DHARAU kwenye ndoa ni mbaya sana..kinyume cha dharau ni HESHIMA!..
So, mtu anapokudharau maana yake hakuheshimu..fikiria unaishi na mtu ambaye kaishakuweka kwenye hii list..how will you keep up?
Halaf dharau inakuja pale ambapo mnakuwa hamna 'common understanding'..yaan kama mwenzio anagundua kuwa wewe haum'fit' kwa lile ambalo mwanzoni alidhani kuwa unaliweza..hapa ndio pale niliposema..'" mjitahidi kufanana misimamo kwenye namna ya kuishi na mipango ya maendeleo kwa ujumla..mingi ya migogoro itapungua..sisemi haitakuwepo!"

Kuachana inategemea na 'extent ya dharau' na kama hakuna jitihada za kuirekebisha..kumbuka ndoa ni Maisha..sasa inakuwa ngumu kuishi kwenye mazingira ambayo unakuwa huna 'AMANI'!!
 

Mkuu SnowBall hapo kwenye hizo red umenena mkuu. Ni kweli changamoto kubwa ni namna ya kuishi ktk ndoa yaani ile daily life, daily treatments ndo wengi tunapobugi step. Na hili ni gumu kulifanyia kazi kwa sababu wengi hatujitambui, hivyo inakuwa ngumu sana kubadilika.

Tatizo la pesa silionagi kama ni shida kubwa, ingawa juzi juzi liliibuka kama issue kwenye ndoa ya rafiki yangu. Hapa jamvini pia mwali ametoa results za utafiti wake.
 

Exactly mkuu (hapo kwa red). Actually hiki ndo nilichokuwa najaribu kukieleza wakati nafafanua kuhusu chanzo cha dharau. Yaani ulivyodhania kumbe sivyo ilivyo, wenyewe wanasema when your expectations perish dharau inaweza kuingia!
 
...... Nimeandika haya kufuatia mazungumzo na baadhi yao kama mimi ambao wameshakata tamaa kuoa kutokana na changamoto kadhaa za wazi wanazoziona kutoka kwa waliooa.
.....


platozoom nasikitika sana hii mada nyeti uliirusha nikiwa nafaidi wkend na hivyo kukosa muda wa kufungua JF na kuangali yaliyojili.

Tukirudi kwenye mada, ni mengi sana mazuri yamechangiwa na wachangiaji wa awali na ningependa kuyaunga mkono maoni yao kwa asilimia kubwa. La kuongeza ni hapo kwenye bold kuwa si jambo jema sana kukataa tamaa ya kuingia kwenye mahusiano kwa kusikia matatizo ya migogoro toka kwenye midomo ya watu. Nimewahi kuzungumza mara nyingi sana kuwa siku zote mabaya ndiyo huvuma zaidi kuliko mema na hapa naamisha wenye migogoro ya ndoa ambao ni wachache ndiyo wanayozungumzia sana matatizo ya migogoro yao ya ndoa na kuifanya taasisi nzima ya ndoa ionekane kama vile haifai au haibebeki kwa manung'uniko yao walio wachache.

Kwa kusema hivyo, ni vyema sana na tena inapendeza mbele za Mungu na binadamu wote ya kuwa kila mume/mke na awe na mwenza wake. Cha kuzingatia ni kuhakikisha kuwa unafahamu in advance changamoto za ndoa, namna ya kuepuka na kutatua migogoro, njia za kubaini na kuwaepuka wachonganishi, namna ya kuboresha ndoa na mahusiano, wajibu wako kama baba ndani ya familia, uelewa juu ya mahusiano, chaguo sahihi la mwenza wako, uvumilivu, uaminifu, kuheshimiana, kusaidiana, kujaliana na mengineyo mengi yanayofanana na hayo. Zingatia pia kuwa hatma ya ndoa ipo kwenye mikono yenu wawili na nyie ndiyo mnaweza kuamua ndoa yenu iwe tamu au chungu kwa kuipalilia vyema au kuacha magugu yaote na kuidhoofisha na baadaye kuiua kabisa.

Ni muhimu kuwa na ndoa ili uweze kuwa na familia yenye watoto wenye furaha na amani huku ukiijenga ktk misingi ya upendo na uaminifu. Ni ngumu sana kuwa na familia yenye upendo wa kutosha kama baba utakuwa mtu wa kuzaa nje hovyo hovyo kwa kuogopa kuingia kwenye ndoa. Ndoa pia huleta ushirika na kusaidia na heshima dhidi ya jamii iliyokuzunguka.

Changamoto mnazoziona kwenye ndoa za baadhi ya watu zisiwakatishe tamaa hata kidogo maana yako mengi mazuri kutoka kwenye ndoa zilizosimama ambao wanandoa huwa hawazungumzii. Lakini laita kama wangelikuwa na wenyewe wanazungumza kama hao wenye migogoro, leo hii ungekuwa tayari kwenye ndoa!:smile-big:

Ngoja nimalizie kazi za jtatu, nitarudi kumalizia mchango wangu kwenye uzi wako!
 
Siri moja ya msingi kabisa katika maisha ya ndoa ni kuhakikisha kila mmoja wenu anamsoma mwenzake na kujua udhaifu na uimara wake.
Kuingia kwenye ndoa ni jambo zuri, lakini unatakiwa kuwa makini na aina ya mtu ambaye unamchagua ili awe mume au mkeo, kwa sababu si kila mtu anafaa kuishi katika maisha ya ndoa. Zingatia sana.
Kwa nini hakuna ndoa isiyo na migogoro hata kidogo? Nini kinashindikana kuwa na ndoa yenye amani siku zote? Si mnapendana kabisa? Ugumu uko wapi? Hapa chini kuna sababu ambazo zinachangia kutokuwepo na ndoa isiyokuwa na migogoro hata kidogo.
ASILI YA KILA MOJA
Kila binadamu ana asili yake ambayo ni tofauti na mwingine. Uchoyo, uchafu, hasira na uropokaji ni mifano ya asili ya kibinadamu. Japo katika maandiko matakatifu tunajifunza kuwa asili yetu sote ni kwa Adamu kama binadamu wa kwanza kuumbwa na Mungu (Imani ya kidini), ni ukweli usiopingika kuwa tunatofautiana kwa mambo mengi.

Hapa naingia moja kwa moja katika asili ya makabila, mila, miiko na desturi ambazo tunakutana nazo katika makuzi tunayopitia kabla ya maisha ya ndoa na jinsi ambavyo huchangia migogoro katika ndoa.
Sasa unakuta kila moja wenu amefundishwa maadili tofauti juu ya kitu fulani, mfano labda katika kabila fulani ni mwiko kabisa kuongea wakati wa kula, au hairuhusiwi mwanamke kula kichwa cha samaki, pengine ni marufuku kulala ukiwa mtupu. Sasa kwa mila na miiko hiyo, unakuta ni tofauti kabisa na ya mwenzako.
Tofauti hizo za kiasili ndizo unakuta zinachangia migogoro ya hapa na pale maana kila mmoja wenu anakuwa na asili tofauti ya mila na desturi pamoja na miiko. Hivyo basi, ni lazima kuna mahali mtatofautiana tu na ndiyo maana nikasema kuwa hakuna ndoa isiyokuwa na migogoro hata kidogo.
Sasa umeona jinsi tofauti za asili zinavyoweza kuleta migogoro? Basi tuingie kwenye sababu ya pili.
FAMILIA
Katika familia kuna malezi na mafunzo mbalimbali yanayotofautiana kutoka moja hadi nyingine. Hapa ndipo kwenye msingi mkubwa kabisa katika kipengele cha kuwa na mwenzi sahihi wa maisha.

Malezi ya familia huchangia mtu kukua katika msingi bora wa maisha au kutokuwa na maadili mema, ndiyo maana ukikuta mtu ana tabia mbaya katika jamii, basi watu huanza kuuliza hivi huyu amelelewa katika familia ipi? Hata zamani mtu akitaka kuoa au kuolewa, jambo la kwanza kabisa ni kuchunguza familia ambayo mwenzi wake anatoka na wakati mwingine uchumba ulikuwa unakufa kabisa kutokana na utofauti wa malezi na misingi ya familia.
Kwa hiyo mkiwa katika ndoa, migogoro mingine hujitokeza kutokana tu na tofauti ya malezi na maadili ya kifamilia. Mathalani katika familia yenu wewe mwanamke, mlikuwa na mazoea ya kula chakula cha mchana saa 8 mchana na cha usiku saa 3, sasa unakuta hali ni tofauti kabisa na familia ya mume wako ambayo ilikuwa na kanuni ya kula saa 6 na saa 2, tayari hapo kunakuwa na mgongano fulani ambao msipouwahi unaweza kuwa ni tatizo.
Kwa hiyo tofauti ya malezi ya kifamilia, huchangia kuibuka kwa matatizo ya hapa na pale katika ndoa nyingi hasa pale mnapokuwa na watoto maana kila mmoja wenu atajaribu kuingiza malezi aliyofudishwa katika familia yake na mwenzako anaweza kuyaona hayafai na ni upotoshaji wa maadili. Kinachofuata hapo ni mabishano na migogoro kama siyo mitafaruku.
MAZINGIRA
Kabla ya kuishi katika ndoa, tunapitia mazingira tofauti kila mmoja wetu kwa mfano shuleni, mitaani na hata nyumbani ambapo unakutana na aina tofauti ya kuishi kama ulivyofundishwa na wazazi wako.

Aina ya watu ambao unakutana nao katika kipindi cha kuingia katika utu uzima ndiyo huchangia kwa kiasi kikubwa kuharibu au kutengeneza maadili ya ukuaji wa mtu.
Aidha, kabla na baada ya kuoa au kuolewa mazingira unayokutananayo yanaweza kukuharibu na kukusababishia matatizo katika ndoa.
 
HorsePower nimekupata barabara kimsingi nimekuelewa sana kwenye haya


Na kifupi umeeleza kwamba ndoa zinaogopwa kwa sababu mabaya kuzihusu husikika zaidi kuliko mazuri. Nafahamu kuna wengine wamezungumzia hili pengine na wewe ungeeleza zaidi ni changamoto zipi zaidi huwepo kwenye ndoa na pengine namna nyingine ya kuzitatua ukiacha ulilosema la kutosikiliza maneno ya nje. Lakini pia kwa kuzingatia kwamba si rahisi kumjua kiundani mwenzi wako kabla ya kuoana..............na kuwa mko kwenye ndoa umegundua madhaifu yake mengi unafanyaje?

Na kwa Nakshi pia nafikiri naye angeongezea nyama zaidi kutokana post yake hasa namna ya kukabili changamoto, hasa unapogundua tofauti kubwa mlizonazo ndani.
 
Last edited by a moderator:
Mie nakuamini kabisa.

Bado kuna wanawake wachache waaminifu 100% japo huwa hawasemi hadharani.

:busu

 

Kwa upande wa changamoto niongezee tu pale wenzangu walipoishia kuwa mojawapo ya changamoto ni Mabadiliko ya tabia baada ya kufunga ndoa. Mara nyingi kabla ya kufunga ndoa, wapenzi wengi hujitahidi kuishi artificial life, kwa lengo la kumpendezesha Mpenzi wake ili wafikie malengo ya ndoa. Kwa mfano, kama ni mdada atajitahidi kuwa msafi, kukupikia unapoenda kumtembelea, kujifanya anapenda sana ndg zako, anaweza kujifanya mkarimu sana, mtoaji, heshima, mnyenyekevu nk. Watu wa namna hii wakiisha ingia kwenye ndoa na kukaa muda fulani hufungua makucha yao na kuonyesha bayana tabia zao za asili. Jambo hili hukera sana na linaweza kuletea ndoa kuvunjika.

Ufumbuzi wa changamoto hii ni mgumu na unahitaji hekima sana kutatua. Ni vizuri kukaa na huyo mkeo na kumshauri kwa upole mwingi na upendo ya kuwa ulimpenda kwa sababu ya tabia fulani nzuri alizozionyesha kabla ya ndoa. Jionyeshe wazi kufurahi sana yale mambo ambayo wewe unayapenda na jionyeshe kuhuzunika sana na zile tabia ambazo wewe hupendezwi nazo. Labda with time mkeo anaweza kuaanza kubadilika taratibu.

Ni vigumu pia kuzijua tabia za mpenzi wako kwa undani kabla ya kuanza kuishi naye. Lakini kukaa kwenye uchumba kwa muda mrefu kwa ukaribu, kushirikiana na ndg zake wa karibu na marafiki, kutembelea mara kwa mara maeneo anayoishi au kufanyia kazi kunaweza kuwa msaada (Japo si sana) kwa watu kukufahamisha tabia za asili za mtarajiwa wako (Hapa inahitaji hekima kujua neno lipi lina nia njema na lipi linaweza kukuharibia mahusiano)

Kuna changamoto zingine kama kubaini kuwa alishazaa nje ya ndoa na alikudanganya, au ni mlevi wa kutupwa, muhuni, mvivu na mshari, hapendi ndugu wa upande wako, na mbaya zaidi kuna mwingine aligundua baada ya kuoa kuwa mkewe pia ni mtumiaji wa 0713! Mambo kama haya hayana formula ya moja kwa moja ya kuyatatua, inategemea na level ya upendo na uvumilivu baina yenu.

Ni vizuri kumuomba Mungu sana wakati wa zoezi hilo la kumchagua mke maana mke siyo gelfriend wa kusema utakuwa naye leo na kesho unaweza kummwaga wakati wowote ....:A S cry:
 

Mtambuzi kuna watu wengi sana wanahitaji ushauri huu naomba uniruhusu nii copy and paste niwatumie baadhi ya watu ambao watahitaji sana ushauri huu...au iko copyrighted??:happy:
 
Hilo la kumfahamu vizuri mchumba wako kwa kukaa nae muda mrefu naliunga mkono asilima 150%. Mimi nimekuwa na mume wangu kwa miaka 4 kabla ya kuoana. Ila tulikuwa wachumba only 6 months kabla ya ndoa. Inabidi vijana mtulie kwenye relationship kama unaona uliye nae ndie na kama sie stop wasting time chapa lapa. Si lazima uwe na mchumba miaka 4 kwani ni mingi kwa uchumba ila ni michache kwa urafiki. Ubaya wa uchumba muda mrefu inakuwa soo ukija vunjika...kwani mnakuwa mliwekeana giza na kuwekeana gundu in life; inabidi mchumbiane pale tu mnapojua mko tayari kwa ndoa.

Kwa experience yangu watu wengi wanafunga ndoa na watu waliokutana ndani ya mwaka...what a risk??? Nina mifano ya ndugu zangu wa karibu eti mtu anakuja home baba nimepata mchumba...hivi hao wachumba wanapatikana wapi? Wengi wanaangalia sherehe badala ya kuangalia ni jinsi gani wameweka maisha yao rehani kwa kucheza kamali ya kufunga ndoa na mtu ambaye humjuhi.


Na kama wengine walivyosema kuna watu maisha ya ndoa hawayawezi; lakini ni wachache sana watu wa hivyo...tatizo kubwa ni kuwa ndoa zenye migogoro sugu ni za partners ambao ni incompatible; ndio maana unaweza shangaa wakitengana kila mtu ana fanikiwa kwenye new relationship
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…