Nyani Ngabu kila lugha ina wazee wanailinda hiyo lugha isije badilika kabisa na kuwa na lugha ingine
nna uhakika kamusi za UK zina tofauti na kamusi za USA
kwa vyovyote vile watu wa UK kuna baadhi ya misamiati watakuambia ya kwao ndo 'sahihi'
hata kama yaliyo popular ni ya USA......
Unachozungumzia wewe ni lahaja, ambayo ni tofauti katika matamshi, maumbo na matumizi ya maneno katika maeneo mbalimbali kwa lugha yenye asili moja.
Lahaja ni jambo la kawaida sana na hata kwenye Kiswahili lipo. Ushawasikia Wamvita au Wazanzibari wakitamka neno 'hospitali'?
Na tofauti kati ya Kiingereza cha Uingereza na kile Kiingereza cha Marekani inajulikana wazi na inakubalika na ndo maana kamusi nyingi za Kiingereza huwa zinatoa maelezo ya tofauti ya matumizi, tahajia, au matamshi kwa yale maneno yaliyo na tofauti baina ya hizo lahaja mbili.
Hata Kiingereza kitumikacho Australia, New Zealand, na Canada nacho kina tofauti zake na kile kitumikacho Uingereza na Marekani.
Hata Kireno kinachotumika Ureno na kile kinachotumika Brasil kiko tofauti na tofauti yake ni ya kilahaja.
Vivyo hivyo, Kihispania kitumikacho Hispania na kile kitumikacho Mexico kina tofauti zake.
Na wala tusiende mbali, tubaki hapa hapa Tanzania. Hivi unajua kuwa Kisukuma kitumikacho Shinyanga, Simiyu, na Mwanza kina tofauti zake?
Wewe kwa mfano waweza usimjue Mnyantuzu akiongea Kisukuma lakini mimi nikimsikia tu najua moja kwa moja huyu anatokea Bariadi.
Kwa hiyo lahaja ni jambo la kawaida kabisa katika lugha.