Badala ya Bunge kuwa mtetezi wa wananchi, limekuwa mbunifu mkuu wa kunyonga Wananchi

Badala ya Bunge kuwa mtetezi wa wananchi, limekuwa mbunifu mkuu wa kunyonga Wananchi

pakaywatek

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2014
Posts
4,660
Reaction score
6,282
Alitoa hoja bwana Zungu kuwa wananchi wachangie serikali kupitia line za simu bila kujua kuwa tayari wanachangia kupitia kununua vocha na kutuma na kupokea pesa.

Sasa zungu akatoa hoja nyingine ya wananchi kulipishwa mara mbili kwenye huduma moja, yaani pale unapotuma hau kutoa pesa kuna kodi ya ongezeko la thamani hiyo inamwangukia mlaji moja kwa moja ndiye mlipaji.

Zungu akaona hiyo haitoshi, akaleta hoja ya kulipishwa kodi ya kichwa kupitia miamala ya kutuma na kupokea pesa ambayo haieleweki huwiyano wake, na serikali ikapokea na kubambikizia wananchi.

Hili bunge badala ya kutoa hoja ya kuwapa nafuu wananchi wamegeuka watafta mbinu ya kuwakomoa wananchi. Ndugai na genge lake ambao hawakuchaguliwa na wananchi wanawakomoa wananchi ili kulipiza kisasi kwa kutowachagua hili halikubaliki.
 
Ni muda wa wananchi kula bakora za shingo, kwani ni wanyonge, ikiwa ni mbadala wa kuwanyonga kabisa.
 
Hao Wabunge hawakuchaguliwa na wananchi, yaani walipitishwa kwa hiyo tusiwalaumu wako sawa.
 
Ndugai akija atauliza, hivi yeye alikuwa wapi? Wakati tozo hii inapita [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Bunge la ndugai limelaaniwa, Wagogo tu wenyewe huwa hawaeleweki Sasa kumpa uspeaker mgogo ndo tulichemsha kabisa, hafu na huyo zungu si huwa muuza madawa ya kulevya aliyejificha huko CCM hawezi jali wananchi kamwe.
 
Acha kuwa mjinga kwa makusudi! Kwani bunge hili ni bunge la wananchi? Kwani hili bunge limechaguliwa na wananchi? Si linamtumikia alielipa ridhaa ya kuwa bungeni?
 
Wameshindwa namna ya kukuza uchumi. Ubunifu umewaishia/hawana. Wanaona njia pekee ya kupata pesa ni unyang'anyi.
 
Neno "WANYONGE" hichi ndio kigezo kikubwa kinacho tukandamiza, kutuonea, na kutuumiza sisi wananchi!

Tukatae tusikubali kuitwa "WANYONGE"

UNYONGE ni kitu dhalili sana kinadhalilisha na kinahuzunisha!
 
Tatizo la kuwa na watu Ombaomba ambao maisha yao ni kuwa na kopo tu
 
Nani ahangaike na wananchi? Halima mdee wako bungeni unadhani kwa ajili ya nini?
 
Alitoa hoja bwana Zungu kuwa wananchi wachangie serikali kupitia line za simu bila kujua kuwa tayari wanachangia kupitia kununua vocha na kutuma na kupokea pesa.
Haya ni matokeo ya Uchaguzi wa Serikali za mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu 2020 chini ya utawala dhalimu wa Magufuri.
 
Hao Wabunge hawakuchaguliwa na wananchi, yaani walipitishwa kwa hiyo tusiwalaumu wako sawa.
Walihesabu kura wakakuta hakuna aliyeshinda sasa wanalipa kisasi
 
Ni muda wa wananchi kula bakora za shingo, kwani ni wanyonge, ikiwa ni mbadala wa kuwanyonga kabisa.
Upigaji wa kura ni kanya boya,yaani ni upuuzi mtupu ,CCM hawajui kwamba kuongoza jamii ambayo haijakupa ridhaa ni kazi kubwa 'you can not be supported' katiba mpya ndiyo mwisho wa matatizo
 
Toka lini bunge la kuteuliwa likawa na tija. na CCM huwa hawana aibu kabisaaaa! hata uchaguzi ujao watarudia hayohayo. mtalaumu na kulaani lakini wao wanasonga mbele.
 
Back
Top Bottom