Badala ya kujali kuporomoka kwa maadili tunajali kuvujishwa siri za watu wa ovyo

Badala ya kujali kuporomoka kwa maadili tunajali kuvujishwa siri za watu wa ovyo

Poppy Hatonn

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2021
Posts
3,095
Reaction score
4,632
Nashangaa sana kiongozi anaposema siri zisivujishwe. Kama kiongozi hataki siri zake zisemwe wapo henchmen wake watahakikisha kwamba siri zake hazisemwi.

Lakini haifai kiongozi kwa matatizo yake binafsi, kwa matatizo ya udhaifu wake wa maadili, ashawishike kutunga amri ya jumla, ya kuihusisha nchi yote kusema siri za watu zisitajwe.

Dunia inaongozwa na siri. Kila kitu kina siri. Kila mtu ana siri. Na siri za mtu ndio zinaamua jambo gani litamfika. Wahindi wanaiita "karma."

Siri ndio inayoamua kwa nini ndege moja inaruka salama,nyingine inaruka na kuanguka. Unasema vipi watu wasitoe siri ?

Tunazungumzia kusema siri za watu, watu wanaokusumbua, wanasema umefanya kosa fulani, kumbe wao wamefanya kosa hilo mara nyingi zaidi. Kwa hiyo unazungumza siri unawaumbua wanafiki.

Halafu ukiitaja ile siri, mtu anakushukuru,anasema,"Aisee, asante kwa kusema hivyo, yule jamaa amenisumbua sana na shutuma zake". Ndio tunasema, mambo yanasemwa because people have a right to know.

Kwa mfano Musiba alikuwa anawapa watu vitu adimu, habari za kiintelijentsia, sasa amepigwa vita, sasa hivi hatujui hata kama yuko hai.

Kweli unahitaji siri katika mambo ya serikali, kwa sababu mipango ikifichuka, inakuwa haitekelezeki, kama vile wezi wakijulikana wanakwenda kuiba benki, wakienda pale wanakuta reception committee. Lakini siri za kuwasitiri tu watu wenye roho dhaifu haifai. Halafu, hawa watu hawajiamini tu, maisha bila kutenda matendo ya aibu yanawezekana.

Nasema hivi, kwa sababu tatizo ni kwamba kiongozi ni mwanamke, ana panic kuhusu siri zake halafu anashawishika kutunga sheria ambazo litalipotosha taifa.
 
Wapigaji hua wanapenda kufanya upigaji kwa siri tatizo wanapiga mali za Umma lazima siri zivuje.
 
Back
Top Bottom