Wengi humu V8 wanaziona barabarani tu hawajui nini kinaendelea. Kuna mahali nili supply brake za mbele na nyuma za 2015 VW Touareg bill ilikuwa 480,000/- na hapo hapo kuna mtu aka supply front brake pads tu za V8 nafikiri ilikuwa 2012/14 hivi mkeka wake ni 400,000/- sikuamini.
Best friend wangu ana Y62 kanunua brand new Nissan hapo, sasa hivi haina hata 20,000km ina wobble ukishika brake, uchunguzi umeonesha ni brake disc zishalika bill 1.2m kila moja na haziko kwenye warranty. Hio gari ikienda service kuacha 800,000-1,200,000 ni kawaida sana.