Badala ya Kutangaza Makusanyo ya Kodi Serikali Itangaze Mauzo ya Bidhaa Nje ya Nchi Kila Mwisho wa Mwezi

Badala ya Kutangaza Makusanyo ya Kodi Serikali Itangaze Mauzo ya Bidhaa Nje ya Nchi Kila Mwisho wa Mwezi

Pang Fung Mi

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2022
Posts
6,653
Reaction score
13,919
Taifa hili kuna eneo muhimu linafumbiwa macho hasa taarifa za Mauzo ya Bidhaa Nje ya Nchi.

Ni vema Serikali hasa Wizara ya viwanda na biashara na msemaji wa ikulu pamoja na yule wa Serikali, waanze mara moja kuweka takwimu za Mauzo na pesa za kigeni kwenye mazao na bidhaa mbalimbali

Kama ilivyo kwenye goods classification ya imports vivyo hivyo hata kwa exports iwekwe bayana kwenye taarifa zao.

Na hii itasaidia wananchi pamoja na wasomi wachumi kuhoji, kushauri, kuhimiza, kutia hamasa, kuibua vikwazo, na mengineyo ikiwa sifa, na mikakati.

Tupate takwimu za bidhaa za viwandani na mazao ya aina mbalimbali mfano. Mauzo ya

1. Kahawa
2.Pamba au nguo vitenge, kanga, vijola etc
3. Korosho
4. Mchele
5. Ufuta
6. Alizeti
7. Choroko
8. Mbaazi
9. Zao la Chai
10. Zao la mpira (rubber)
11. Mahindi
12. Mbaazi
,13. Maharagwe
14. Samaki na Dagaa
15. Cocoa
16. Mawese
17. Parachichi na jamii za matunda mfano Maembe, Nanasi, Tikiti maji, Machungwa
18. Tangawizi na jamii za viungo vya mapishi
19. Karafuu
20. Zao la hiliki
21. Madini
21.Mazao ya misitu miti, mbao, Asali na etc
22. Mauzo ya nyama mfano huko Comoro na etc
23. Mauzo ya vitunguu, nyanya etc
23. Mauzo ya karoti na Maua

Naomba kuwasilisha
Ntarudi baadae kuendelea na nondo

Wadiz
 
Kwenye uchumi only exportation ndio inalipa na kuokoa uchumi wa mataifa mengi, nakuunga mkono hiyo itatia hamasa hata wajasiriamali kutanua uwanja wa utafutaji na wawekeze wapi kwenye tija
 
Back
Top Bottom