Badala ya Vyama, Wapiga kura ndio tupewe pesa ya posho

Badala ya Vyama, Wapiga kura ndio tupewe pesa ya posho

paul sylvester

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2020
Posts
3,503
Reaction score
3,504
Tulikotoka ni mbaali saana, tuendako ndio mbaali zaidi.

Tumekuwa na uchaguzi wa kila Baada ya miaka mitano tunachagua viongozi wetu Kwa mjibu wa katiba yetu na ni haki ya kila Mtanzania mwenye kutimiza vigezo vya kupiga na kupigiwa Kura hufanya hivyo.

Tuliko toka tumekuwa na chaguzi zenye kusisimua na zilizovutia wapiga Kura weeengi sana wamekuwa wakijitokeza kuwapigia Kura viongozi wao.

Leo, ni tofauti kabisa,mbi na wananchi kuhamasishwa kujitokeza Ili kwenda kupiga kura, unajua Wahenga ni watu walioona mbali Sana, walisema, Nyota njema huonekana Asubuhi.

Nimedamka asubuhi kabla hata ya vituo kufunguliwa Mimi nikaweka foleni yangu kuhakikisha kuwa ni lazima niwe mtu wa Kwanza kupiga Kura.

Kabla ya muda kufika, foleni yangu nikajikuta iko na wazee weengi Sana kiasi kwamba nikaamua niwapishe wao wawe wa Kwanza kupiga Kura Kwa sababu Mimi bado damu changa.

Nimemaliza kupiga Kura saa 2:03 hivi nikiwa mtu wa Ishirini na usheee hivi.

Na nilipo maliza kupiga Kura muda michache tu kukawa hakuna watu kabisa hapo kituoni, Nimejaribu kutembelea pia vituo vingine vingi lakini nako hakuna watu, na wengi wa waliojitokeza kiukweli kabisa ni watu wenye umri wa juu, vijana sjajajua labda muda utasema.

Nachotaka kushauri Hapa ni Kwa Serikari yetu, Kwa jinsi tunavyokwenda, ni Bora sasa pesa zinazotumika Kwa ajiri ya vyama kujinadi katika mikutano mbalimbali nchi nzima, ni Bora sasa hizo pesa zielekezwe Kwa wapiga Kura, kwamba, kila mpiga Kura siku hiyo atalipwa kiasi Fulani ili sasa kuwavutia wapigakura wengi nyakati za uchaguzi mkuu.

Kuna watu ambao Kwa fikra finyu, hudhani kwenda kupiga Kura ni kitendo cha kwenda kumpa mtu ulaji bila sababu yoyote, mwingine hudhani, hata akipiga Kura, mambo yatakuwa ni hayohayo, na mwingine huwaza mbaaali sana, kitendo cha kufunga kazi zake kwenda kupanga foleni asiingize chochote siku hiyo huku akili yake ikimtuma kuwa, anayekwenda kumchagua, mshahara wake tu wa mwezi mmoja unaopatikana kutokana na Kura yake ni mkubwa kiasi kwamba yeye hawezi kuipata hiyo pesa hata Kwa kipindi chote cha miaka mitano atakayokaa kwenye Uongozi.

Kwa namna hiyo anaamua kupotezea

Kwa hiyo, serikali yetu, kama itaona vema, badala ya pesa nyingi kutumika kwenye Kampeni tu, basi pesa hiyo siku ya uchaguzi itumike kama posho Kwa kila mpiga Kura, hiyo itavutia watu wengi kupiga Kura.

Na badala ya vyama kuzunguka nchi nzima kupiga Kampeni na matokeo yake ni kidogo Kwa wapiga Kura, basi vyama viwe vinaendesha Kampeni kwenye Mitandao ya kijamii pekee na kwenye luninga ili kusevu pesa ya walala Hoi kutumika kusikoleta badriko na hamasa kwa wapiga Kura.

Asante
 
Watu wamekuwa hawana mwitikio kabisa, ni Bora Ile pesa ya uchaguzi, iwe ni posho Kwa wapiga kura
 
Ha ha haaaaaaaa
leo kumekucha hayo wengine hatupo huko.. tunasubiri kutangazwa tano tena za Rais wa Dunia

Magufuli.. 💛 💚 💛 💚 💛
 
Kwenye Kampeni watu ni wengi, kwenye Kupiga Kura hakuna, Bora kuwepo posho siku ya uchaguzi Kwa kila mpiga kura
 
Back
Top Bottom