Badala ya Vyeti kutofanya vizuri mtaani nimeanza na hii business (Party and rental Items )

Badala ya Vyeti kutofanya vizuri mtaani nimeanza na hii business (Party and rental Items )

Waibi fredy

Senior Member
Joined
Jul 4, 2018
Posts
194
Reaction score
227
Habari ndugu zangu.
Badala kukaa kipindi kirefu benchi na pirika kutafuta ajira
Nimekuja na hii Idea (Party and rental Items ) maswala ya upambaji .Hii business nzuri sana na yenye faida nzuri kwa mwenye kukodisha vitu na yule mpambaji .

Tuanze na mkodishaji vitu - huyu mtu mtaji wake ni vifaa tu mfano viti , meza ,tent, backdrop za kupambia ,light n.k
Mfano meza moja round na viti kumi anakodisha kwa 15,000/= let say mteja (mpambaji ) ana Idadi ya watu 250 sawa na meza 25 = 375,000/= usafiri juu ya mteja (mpambaji)
Bado glass
Sahani
Taa za ukumbini n.k so unaweza kuona anachukua profit kubwa kwa wakati mmoja tu .. mara nyingi hawa huwa awapambi ukumbini

Mtu wa pili
Mteja ( mpambaji ) - mtaji wake na silaha yake kubwa kwenye bajeti ya mteja wake lets say mteja wake bajeti yake 1.5m katika hiyo bajeti atatoa gharama za kukodisha vitu na usafiri (go and return ) kinachobakia ndio faida yake .

Changamoto inakuja wateja pasua kichwa wanaitaji vitu vingi bajeti ndogo mwisho wa siku mpambaji anajaza Taa ukumbi mzima bila ya kuwa ubunifu wowote ili aweze pata faida .

Napenda kuwashauri vijana wenzangu tuwekeze kwenye hii kazi na tuwe wabunifu watu kila siku watu wanazaliwa , wanafunga ndoa, arobaini za watoto, kipaimaira , graduation ,open day so hizi zote ni fulsa lazima tuzichangamkie .

Asanteni
Screenshot_20220623-150213_WhatsApp.jpg
Screenshot_20220623-165242_Instagram.jpg
Screenshot_20220623-145757_Instagram.jpg
Screenshot_20220619-152639_Instagram.jpg
Screenshot_20220614-225131_Instagram.jpg
Screenshot_20220614-225816_Instagram.jpg
Screenshot_20220608-220755_Instagram.jpg
 
Kusema ukweli hii biashara ni ngumu sana yaani mara 100 anayefanya biashara ya kuonesha mpira kwenye mabanda umiza ana uhakika wa kupata hela kuliko hii.

Assume mtaani kwako hakujatokea msiba wala sherehe kwa mwaka mzima utaishi vipi?

Hii biashara inawafaa matajiri wenye biashara nyingi kisha ananunua hayo makolokolo anayafungia store anayasahau kabisa anakuwa bize na biashara zake zingine kisha mwaka wowote mtakaopata sherehe mtaenda kumtafuta.
 
😳 😳 😳
 
Sio kweli kabisa kafanye research upya fatilia wanakodisha vitu vya masherehe usiwaze tu msiba kukodisha maturubai. Kuna vitu vingi vya kukodisha na kila siku watu wanasherehe labra ujafanya research ya uwakika .

Back
Top Bottom