Badia za kunde

Nilikuwa sijui kama kuna za kunde pia, lakini nilishawahi kula mahali zilikuwa tamu kuliko kawaida nadhani ndiyo hizo za kunde.

Yeah ni hizo...tena zile wanaopika mama zetu za kutwanga hizo kunde tamu zaidi....
Ila siku hizi mambo ya technolojia haya yanatufanya tuwe wavivu....
Mie chapati za maji nkiwa na haraka zangu nachanganya kwa handmixer lol....
 
Mie nnavojua ni badia... za kunde tamu zaidi BAK...kwa chatne ya nazi au hiyo ya embe mbichi weee utamu hadi machoni lol...

Wewe bidada mimi maneno yako tuu yananiachaga hoi na kunifanya nijione sifahamu kiswahili fasaha. Maana mara badia, uzile, thomu n.k ukijumlisha na mahanjumati unayoyawekaga ndio kabisaa nabaki hoi.
 
Last edited by a moderator:
Naomba nisaidie vitu vifuatavyo vyaitwaje in English:
Kunde (za kupaa/za lubya)
Dengu
Choroko
Mbaazi
Gilgiliani
Pilipili manga
 
Ukila uwe na glass na maji pembeni au maziwa lol..
Wenzio humu ndani kutwa twaasumbuliwa na heartburn kwa mapilipili lol...
ha ha ha halafu hukomi bado umekomaa nayo tu...Ukienda msalani si ndoo balaaa!!
 
Wewe bidada mimi maneno yako tuu yananiachaga hoi na kunifanya nijione sifahamu kiswahili fasaha. Maana mara badia, uzile, thomu n.k ukijumlisha na mahanjumati unayoyawekaga ndio kabisaa nabaki hoi.

Wajua vizuri kiswahili...ila kuna viswahili vingi hapo kila mtu ana chake wewe ukiwa hufahamu kitu uliza wengine watakusaidia kiswahili ambacho wewe utaelewa...mfano shosti mimi49..
 
Last edited by a moderator:
Naomba nisaidie vitu vifuatavyo vyaitwaje in English:
Kunde (za kupaa/za lubya)
Dengu
Choroko
Mbaazi
Gilgiliani
Pilipili manga

Dengu-chickpea..
Pilipili manga-black pepper
Giligilani -koriander
Mbaazi-pigeon peas
Choroko-small green beans
 
Wajua vizuri kiswahili...ila kuna viswahili vingi hapo kila mtu ana chake wewe ukiwa hufahamu kitu uliza wengine watakusaidia kiswahili ambacho wewe utaelewa...mfano shosti mimi49..
Choroko-Mung beans
Giligilani-coriander
Mbaazi-Black eyed beans
Kunde-Adzuki beans
Dengu-Split chickpeas
Pilipili manga-black pepper
 
Choroko-Mung beans
Giligilani-coriander
Mbaazi-Black eyed beans
Kunde-Adzuki beans
Dengu-Split chickpeas
Pilipili manga-black pepper

Mimi49 waujua mvuje? Mimi kutia kwenye badia vijani vyake...ila wengi hawapendi
 
Hivi wewe ni wa Mvita au wa Amu

Nimependa lafidhi yako.
 
Hizi ndo tamu, kuliko zile za dengu. Weekend ijayo itakuwa ya kujaribu mapishi yako kadhaa likiwemo hili. Ntakuonjesha mpishi mkuu unipe alama za ufaulu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…