SoC01 Badili mtazamo wako juu yako na utaona mabadiliko kwenye maisha yako

SoC01 Badili mtazamo wako juu yako na utaona mabadiliko kwenye maisha yako

Stories of Change - 2021 Competition

EliasJoram

New Member
Joined
Jul 16, 2021
Posts
1
Reaction score
3
Waelewe watu usiwahukumu watu

Binadamu hufanya maamuzi kwa hisia alizonazo kwa wakati huo
Akiongea maneno mazuri au mabaya anafanya hivyo kwa sababu ya hisia zake kwa wakati huo sio kwa sababu yako

Hisia zake zikibadilika na matendo yake hubadilika

Kila kitu huanza kwenye fikra na ikiwa mtu hajajiandaa kiakili hawezi kujiandaa kimwili

Alisema Epictetus kuwa "binadamu huwa hajifunzi chochote pale anapoamini anakijua"

Kama utabadilisha mtazamo wako juu ya maisha yako utaona mabadiliko makubwa sana

Kama utatafuta mabaya kwa watu utaona mengi sana na itakuwa sababu ya kuwachukia

Kama utatazama mazuri kwa watu utaona mazuri mengi sana na utawapenda

Alisema Eckor Tolle kuwa "When ego dies awareness begin"

Kama ukiona kuna mtu unamchukia ujue tatizo lipo kwako sio kwake

Huwezi kumpenda kila mtu kwa sababu matarajio yako kwa watu ni tofauti na vilevile huwezi kupendwa na kila mtu kwa sababu matarajio ya watu wengine ni tofauti na tabia yako

Ukiona watu wanavunja ahadi ni kwa sababu wao wenyewe huwa wanajipa majukumu kuliko uwezo wao

Ukiona mtu anatoa ahadi kibao ujue ni miongoni mwa watu ambao huweka malengo mengi sana na huwa hayatimii malengo yao

Ukiona mtu ni mwenye tabasamu sio kwa sababu anakupenda Lah ni kwa sababu anafuraha muda huo

Ukiona mtu ni mwenye hasira ni kwa sababu ya hisia zake kwa wakati huo sio kwa sababu ya matendo yako

Watu hufanya matendo kwa kuongozwa na hisia ndio sababu huonekana na kauli tofauti kila wakati na wengine huwaona ni wanafki sio kweli ni hisia zao ndio HUBADILIKA na kufanya matendo yao kubadilika

Ukiwa na siku mbaya huwa unakuwa na tabia gani kwa wengine?

Labda umepoteza pesa, umechelewa safari,ahadi kuvunjwa,huna pesa au umekwazana na watu njiani matendo yako kwa watu ukikutana nao huwa yapoje?

Utagundua kuwa ukiwa na mood mbaya hata matendo yako huwa sio mazuri hivyo na watu wengine hufanya matendo mabaya kwa sababu ya hisia mbaya za wakati huo

Mtu akiwa na hasira hawezi kukusema kwa mazuri hivyo huna sababu ya kumchukia mtu kwa kukusema kwa ubaya kwa sababu kauli za watu ni kiwakilishi cha hisia zao kwa wakati huo

Ukiwa na haraka huwezi kuwa na uvumilivu na vilevile huwezi kuelewa maelezo marefu kama ukiambiwa usikilize hivyo ukiona mtu hasikilizi vizuri maneno yako sio kwa sababu ya ubaya wa maneno yako bali hisia zake ndio mbaya kwa wakati huo

Ukisikiliza wimbo mmoja kwanzia asubuhi mpaka jioni utaona wimbo huo ni mbaya sana lakini sio kwamba wimbo ni mbaya Lah bali hisia zako kwenye wimbo zimekuwa mbaya

Upendo ukiondoka chuki huanza hivyo ikiwa huna furaha kwa sasa ni kwa sababu ya hisia za chuki zimetawala fikra zako

Badilisha fikra zako utaona hisia zako zinakuwa tofauti

Kama mtu akisema maneno mabaya endapo utaona huo ni uonevu kwako utapata hasira sana lakini ukiona amefanya hivyo kwa sababu ya hasira zake utamuelewa zaidi kuliko kumchukia

Maneno ya watu hueleza zaidi hisia zao wala sio uhalisia wako

Maneno na matendo ya watu HUBADILIKA kwa sababu ya mabadiliko ya hisia zao wala sio mikosi yako au kuwa fungu la kukosa

Ni rahisi kuanza kujichukia sana kama ahadi zikivunjwa utahisi umewakosea watu lakini sio kweli watu huvunja ahadi kama wakiona hakuna manufaa ya kutimiza ahadi hiyo

Ukiwaa na hasira,uchovu, maumivu,ukiwa mgonjwa,ukiwa na njaa,ukiwa umechanganyikiwa,ukiwa ,hofu,woga, wasiwasi,ukiwa umevunjwa moyo sio wakati sahihi wa kufanya maamuzi

Maamuzi ambayo utafanya kwa sababu ya hisia zako utajuta baadaye kwa sababu utapata nafasi ya kubadilisha hisia lakini huwezi kupata muda wa kubadilisha maneno ambayo umeongea kwa sababu ya hasira

Usichanganye maneno mabaya na hisia mbaya kwa sababu hisia mbaya hubadilika lakini maneno mabaya hubaki kwenye kumbukumbu za milele

Kama furaha yako umeiweka kwenye vitu ambavyo sio rahisi kuvipata kama utajiri,cheo, kipato kikubwa, kupendwa, kusifiwa ni rahisi kuteseka sana

Ikiwa furaha yako ipo kwenye maamuzi ya wengine utakuwa mtumwa kwa watu hao kwa sababu wanaweza kubadilisha maamuzi muda wowote

Zipo sababu kibao za kushindwa kufikia malengo yako na matarajio yako hivyo furaha yako iweke kwenye vitu ambavyo ni rahisi kuvipata sio vitu ambavyo ni vigumu

Weka furaha yako kwenye vitu upo navyo kwa wakati huu sio kwa vitu unavyotarajia kuvipata

Kila ugumu kwenye maisha huwa unakuja na nguvu ya ushindi ndani yake

Kama unapata maumivu makali sana tazama kuna kitu maisha yanataka kukufundisha

Tenganisha maisha yako sehemu mbili sehemu unayoweza kudhibiti na sehemu huwezi kudhibiti

Vitu huwezi kudhibiti ni kama vile maamuzi ya wengine,hisia za wengine,tabia za wengine, matendo ya wengine,imani za wengine,mawazo ya wengine

Huwezi kupanga nini kitokee maishani mwako bali unapanga ufanye nini kwa lile limetokea

Kupata hasira kwa sababu ya matendo ya wengine ni kujipa adhabu kwa kosa hujafanya

Hakuna binadamu ambaye anaweza kukuchukia kuliko chuki ambayo unaweza kujichukia mwenyewe

"Best revenge is Love"

Upendo huondoa chuki na chuki huzaa chuki
Jenga tabia ambayo kwa 97% ya watu duniani hawana

Ukiweza kusoma vitabu ambayo kwa 97% ya watu hawawezi kusoma utaweza kuona vitu ambavyo 97% ya watu hawawezi kuona

Ukifanya vitu ambavyo 97% ya watu hawawezi kufanya utafanikiwa kiasi ambacho 97% ya watu hawawezi kufanikiwa
 
Upvote 4
Back
Top Bottom