Bado Hamuuoni Mwisho Wa Diamond?

Bila shaka wakati wa kutakiwa kutoa kafara kubwa umefika.
 
nyimbo za mond nazikilizaga za kitambo tu izi zingine chache sana
 
Hebu tuwekee hilo bit la Jux unalodai kadqndia tulisikie
 

Kila Mwanamuziki anakuwa na Peak yake ,kisha anaanza kushuka.

Kwasasa Dayamondi anabebwa na misukule yake(fan base) ,hawezi kupata fans wapya wakampenda kwasababu ya kazi ,misukule ipo kwa ajili ya ushabiki tu na si kwamba kazi nzuri.
 
Hata mtu akiwa anafirisika anakuwa hivyo,unaweza ukawa na hela bank unabishana nazo hizi haziishi,ukija kushtuka akaunt inasoma 0!
Alivyoanza tu mikwara ya kukaa trending miezi 6 nikajua hapa tayari mwendo ameumaliza,sasa kabaki kuiganda ngoma ya Jux na zake mbili haziongelei kabisa.
Na hii ya kukaa kimya ni uongo,kwani zuwena na yatapita zimetoka lini?
 
Una safari ndefu sana katika kuujua muziki, nyimbo kuwa hitsong si lazima isikike mtaani tu. Mapopo ya mavokali uliwahi kuisikia mtaani au nyimbo ilianza kutembea kwenye digital platforms?

Zuchu aliibuka na tuzo nyingi TMA kuliko msanii yyte yule, je kati ya Zuchu na Harmonize ni msanii gani alikuwa akisikika mtaani sana? Ngoma za Diamond kuanzia yatapita hadi shu zote zimeingia kwenye youtube trending tab za UK, France, Nigeria na USA na akitoa video zinashika charts za juu East Africa nzima, je ni msanii gani umewahi kumuona akifanya hayo?

Unasema kashuka ila kwa mwaka huu tu ndio msanii anayeongoza kuwa nominated kwenye International awards je hao wasanii waliopanda mbona hawafiki huko na kuishia kidimbwi tu. WCB wanapigwa vita na media nyingi tu Tz je wewe km raia utasikiliza wasafi 24/7? Marioo huyo hapo anasikika mitaani kila siku lini umewahi kumuona kapata shows za kimataifa?
 
Kwa hiyo ww unadhani ni nguvu ya Juma pekee Alikiba anavyo angaika kumtoa trending? Hizo yatapita na zuwena nenda katafute video zenye mauzo mengi huu mwaka kuliko hizo yatapita na zuwena. Au tafuta ngoma ya Jux ambayo imewahi kufanya vzr kuzidi hii aliyomshirikisha Mond. Wasanii wengi bongo wanahitaji support ya Mond ndio watoboe ila Mond haitaji support ya mtu yeyote ni yy mashabiki zake tu.
 
Ku drop sishangai na binafsi sioni kama ka drop ila sasa hivi diamond

mziki sio priority yake,nadhan sasa hivi diamond anafanya mziki kwasababu

ni kitu alichoanza nacho na anakipenda ila sio kama zamani enzi anautumia mziki

kuishi na kufanya kila kitu kwa mziki,sasa hivi diamond kawa mfanyabiashara si tu mwanamuziki

ana mambo mengi na hata hivyo kwa upande wangu anajitahidi na bado nitamuona ni no 1

kwa nchi yetu hiii simuoni hata wa kumnukia diamond hata ikitokea amesema leo haimbi tena

Muziki sio kuimba tu,muziki unahitaji kipaji ukipenyeze huko duniani who else kumtoa diamond?
 
Wasanii gani hao walikua kimya maana kina marioo, harmonize, alikiba, jay melody hadi chino wana man walikua wanaendelea kushusha ngoma.
Au labda zilikua ngoma za wasanii wa msumbiji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…