Bado Kenya na Uhuru Kenyatta ni baba wa demokrasia Afrika Mashariki?

Bado Kenya na Uhuru Kenyatta ni baba wa demokrasia Afrika Mashariki?

Hakuna Baba wa Demokrasia wala nini
Kenya kuna Ombwe la mauaji ya Wanasiasa wanao kinzana na Msimamo wa Uhuru
lakini kwa kuwa Watanzania tuna Tabia ya Kufuata mkumbo na ushabiki wa kijinga kizuri cha jirani tu
hili ningumu kuliweka wazi.
Unanikosha sana
 
Mimi naamini, lile jinamizi la utawala mbovu bado limepiga kambi Afrika Mashariki na inavyoonekana litatutesa kwa miaka kadhaa ijayo.
 
Halafu hiyo Namba ya Simu ya nini humu? Au mambo ya uteuzi?
 
Jambo lililonikera ni kubadili sheria ya uchaguzi .....ili tu mahakama isiwe na power ya kufutilia mbali uchaguzi utakapokuwa wa magumashi kama TZ
 
Wewe ni sawa na mwanangu wa kumzaa kwa hiyo ushauri wako wa kiuanasesere unawafaa tu watoto wa rika lako!
Mimi nilikupa ushauri kwa nia njema, kwasababu yule bint Zuwena inaonekana wazi alikuwa anakuzidi kwa mbali sana katika uwezo wa kufikiri pamoja na umri wako kuwa mkubwa, ila kama umeukataa ushauri wangu kwa sababu tu mimi ni mdogo kwako, bila kujali kama ushauri wangu una maana au hapana, ni dalili ya wazi kwamba mkeo na watoto wako nyumbani wanateseka sana kwa kuwa na baba kichwa ngumu kama wewe.
 
Hakuna Baba wa Demokrasia wala nini
Kenya kuna Ombwe la mauaji ya Wanasiasa wanao kinzana na Msimamo wa Uhuru
lakini kwa kuwa Watanzania tuna Tabia ya Kufuata mkumbo na ushabiki wa kijinga kizuri cha jirani tu
hili ningumu kuliweka wazi.

kaka waambie watanzania waache kufata mkumbo kwa kua et magu anataja odinga nani asie jua kua uhuru ana kisea
 
Mimi nilikupa ushauri kwa nia njema, kwasababu yule bint Zuwena inaonekana wazi alikuwa anakuzidi kwa mbali sana katika uwezo wa kufikiri pamoja na umri wako kuwa mkubwa, ila kama umeukataa ushauri wangu kwa sababu tu mimi ni mdogo kwako, bila kujali kama ushauri wangu una maana au hapana, ni dalili ya wazi kwamba mkeo na watoto wako nyumbani wanateseka sana kwa kuwa na baba kichwa ngumu kama wewe.
Misukule ya ccm mnajiwaza mnafikiri kuzidi hata hizo fikra...ukombozi wa pili ukiisha kupatikana wewe na wenzio ni wa kupiga msasa kwanza ili tuondokane na taifa mbumbumbu...
 
Misukule ya ccm mnajiwaza mnafikiri kuzidi hata hizo fikra...ukombozi wa pili ukiisha kupatikana wewe na wenzio ni wa kupiga msasa kwanza ili tuondokane na taifa mbumbumbu...
Kama mkeo tu amekushinda hadi ameamua kuchepuka, mimi sitokuweza
 
Na Bashir Yakub.
+255784482959.

1. Tokea mahakama kutengua matokeo ya rais, serikali iliwaondolea ulinzi mara moja jaji mkuu Maraga na makamu wake Philomena Mwiru. Wawili hawa kwasasa wanalindwa kampuni binafsi za ulinzi walizo ajiri wao wenyewe.

2. Ndani ya wiki mbili ambazo NASA ya Odinga wametangaza maandamamo tayari watu zaidi 35 wameshauliwa na polisi wakiwemo watoto wadogo wawili.

3. Raila Odinga na mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka nao wameondolewa ulinzi maalum kutoka serikalini. Raila anapata haki ya ulinzi maalum kwa mujibu wa sheria kwakuwa ni Wazir mkuu mstaafu na Kalonzo ni makamu wa rais mstaafu.

4. Jimmy Wanjigi ni tajiri anayemsapoti Odinga. Leo ni siku ya tatu amefungiwa nyumban kwake na familia yake na kikosi maalum cha usalama. Mahakama imetoa amri kikosi kiondoke kwake lakini wamekaidi amri hiyo.

5. Leo Kamisha wa tume huru ya uchaguzi Dk. Roselyn Akombe amejiuzulu na kukimbilia Marekani. Anasema serikali inaisukuma tume upande ambao yeye hawezi kuwa sehemu yake.

6. Bunge la Kenya linalooongozwa na Jubilee ya Uhuru limebadili sheria ya uchaguzi ktk kipindi cha uchaguzi ndani ya wiki moja ili itumike ktk uchaguzi huo huo kitu ambacho si tu ni kosa Kenya bali hata kwenye Sheria za Kimataifa .

7. Maandamano ya NASA ya Odinga yamepigwa marufuku kwenye miji mikubwa yote. Mahakama imetoa zuio kutaka maandamano kuendelea lakini serikali imekaidi zuio hilo.

8. Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Wafura Chebukati mda mfupi uliopita amesema hataacha kujiuzulu kabla ya uchaguzi ndani ya siku 6 zilizobaki kulinda heshima yake na familia ikiwa Tume itaendelea kuingiliwa na mamlaka kama ilivyo sasa.

9. Haya yametokea ndani ya wiki tatu na ni mbali na yale ya kabla na baada ya tarehe 8 wakati matokeo ya kwanza yalipotolewa ambapo :
Taasisi mbili za haki za binadamu zilifungiwa.

Vifo ya watu 26 Kisumu.

Kumtishia jaji mkuu kuwa atakomeshwa baada ya uchaguzi, nk. nk.

Je bado Kenya na Uhuru Kenyatta ni baba wa demokrasia Afrika Mashariki ???.
Kwa CHADEMA mbona bado ni demokrasia tu? Unataka sisi wapenzi wa CHADEMA tupate wapi cha kumkosoa JPM? Mnataka tukalie kuangalia tu anavyotekeleza Ilani yao ya CCM, sisi tutawaambia nini wapiga kura 2020?
 
Back
Top Bottom