Hili ndiyo tatizo la kutokuwa na mipango ya muda mfupi na mipango ya muda mrefu kwa vilabu vyetu vikongwe.
-Mipango ya muda mrefu ni kuandaa vijana wa kikosi cha pili, ambao wanaweza kupandishwa daraja, siku za usoni.
-Mipango ya muda mfupi ni kuwa timu ya scouting yenye weledi wa kuona vipaji vya wachezaji wa nje klabu na uwezo mkubwa wa kushawishi na kuingia mikataba yenye tija kwa klabu.
-Kukosekana kwa mipango ya muda mfupi na muda mrefu,husababisha vilabu hivi kusajili wachezaji kwa mihemko na mfumo wa zima Moto ili kuwafurahisha washabiki na wanachama wao
-Mashabiki na wanachama wanaotaka kusikia au kuona wachezaji wapya wanasajiliwa klabuni kwao hata kama hawahitajiki.
-Lakini ukiangalia kuna baadhi ya vilabu vina wachezaji wazuri na wanaweza kuunda hata vikosi viwili bora na wachezaji wote wako timamu,hakuna majeruhi.
-Uhalisia kuna matatizo ya makocha wetu, hawana mbinu na weledi wa kuwabadilisha wachezaji kuingia kwenye mifumo yao na wanatumia kisingizio cha mapungufu ya baadhi ya wachezaji kulinda ajira zao.
-Kuna beki tatu( pro ) wa timu moja karibu afukuzwe, lakini sasa hivi amepata match fitness na kuelewa falsafsa ya kocha wake, na amekuwa tegemeo la klabu na kipenzi cha mashibiki.
Sent from my TECNO KC8 using
JamiiForums mobile app