MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
BADO MBOWE NI KIONGOZI SAHIHI KWENYE HIZI NYAKATI ZA MWISHO WA UHAI WA CHADEMA.
Najua mtashangaa sana kwa huu uzi wa leo. Ni kwamba kama akili kubwa nimeona niliweke hili suala la uenyekiti wa Mbowe. Kuna wanaoona ni sahihi yeye kuendelea kuwa mwenyekiti kwa maisha ya CHADEMA yaliyobakia na kuna wengine wanaoona hata kwa hizi dakika za mwisho wa uhai wa CHADEMA hafai kuendelea kuwa mwenyekiti.
Makundi yote mawili yana hoja nzito. Kabla ya ufafanuzi lazima kwa pamoja tukubaliane hiki Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kiko kwenye hatua za kuumaliza mwendo.
Mimi naungana na kundi la kwanza linaloona Mbowe ni mwenyekiti sahihi kwa hizi nyakati za mwisho wa uhai wa Chama chake. Mbowe ni mwanasiasa ambaye tayari kaweka alama nyingi sana za kisiasa kwenye nchi hii. Kabla ya 2005 alifanya usajili mzito mno wa wanasiasa vijana toka vyuo vikuu na kwingineko nchini hali iliyochangamsha mno kisiasa. Nakumbuka uchaguzi wa 2005 wananchi wengi walivutiwa na kampeni za CHADEMA ila hakukuwa na namna ya kuzidi nguvu ya CCM na mgombea wake JK.
Ule usajili uliwezesha bunge kuwa na vijana machachari sana wakiongozwa na Zitto. Ambao waliibua mambo mengi na kuwaamsha wananchi wengi hivyo kufanya nyota ya upinzani kung'aa. Baada ya uchaguzi wa 2005 chama kilizidi kuchanja mbuga kwa kuja na Operesheni Sangara huku kikiendelea kufanya usajili wa wanachama wengi hasa vijana.
Hadi 2015 CHADEMA kikawa chama kikuu cha upinzani. Lakini yote yalitokea wakati katibu mkuu wa Chama akiwa Dr Slaa ambaye naye aliubeba upinzani mabegani na kuufikisha mbali sana kwa kushirikiana na Mbowe.
Mambo mazuri ya Mbowe ni mengi ila uamuzi wake wa kubadili GIA ANGANI mwaka 2015 ndo ukawa mwanzo wa mwisho wa chama kikuu cha upinzani nchini. Pamoja na hali ya kisiasa kutokuwa rafiki sana kwa wapinzani 2015 - 2020 lakini bado Mbowe aliendelea kuwa mwenye busara na mvumilivu mno haijapata kutokea. Kilichoimaliza CHADEMA ya Mbowe kwa miaka mitano ni wanachama wengi hasa viongozi waandamizi kutokuwa wavumilivu. Wengi wenye akili walihama chama chao na kujiunga na CCM.
Mwenyekiti akabakiwa na viongozi wasioweza kujenga hoja wala kujua muda gani waongee nini huku wale waliokibeba chama wakienda kuwa viongozi kwenye serikali ya CCM. Pamoja na jitihada kadhaa za Mbowe kukiimarisha chama bado hana watu wa kumsaidia hivyo jitihada zake kuwa kama machozi ya mamba.
Mimi ninachoweza kumshauri Mbowe ni kuunga mkono serikali ya Mama Samia huenda akateuliwa kuwa mwenyekiti wa bodi ya Parole ambayo hata Mh Lyatonga Mrema alishawahi teuliwa.