King Jody
JF-Expert Member
- Oct 8, 2022
- 1,834
- 3,456
Habari za kutwa wana jamii forum, Poleni na pilika za kusaka mkate wa kila siku,
Niende moja kwa moja kwenye hoja ya msingi,
Baba na mama walitengana kitambo nikiwa na miaka 2, hivyo sisi tumelelewa na mama pekee,
Mama alikuwa akijishughulisha na kazi mbalimbali kama vile kufanya vibarua kwa kulima mashamba ya watu nk,
Sasa siku moja kwenye mida ya saa 10 tukiwa tunacheza nje mi na dadangu pamoja na watoto mwengine,
Mama alirudi kutoka kwenye shughuli zake, baada ya kula alioga na kulala japo hakuwa na tabia ya kulala mchana.
Sisi tukaendelea kucheza hadi mida ya saa 1 usiku, tukarudi ndani ili tujiandae kuoga,
Mara mama akaamka akachukua jembe, tukamuuliza mama unaenda wapi?, akasema naenda shambani kulima, tukamwambia mama unaendaje kulima usiku? hakutaka kuelewa, alikuwa kama amechanganyikiwa,
Tukaanza kulia huku tunaomba msaada kwa majirani, walivyokuja kidogo mama akili zikarejea akashtuka,
Akaweke jembe chini akabaki anajitafakari.
Huwa namkumbusha ananiambia, dunia ina mambo mengi mwanangu.
Thanks for your time guys.