Bado natafuta connection ili biashara yangu iweze kukua

mxrereco

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2014
Posts
1,906
Reaction score
3,986
Habari wapambanaji...

Katika harakati zangu za kuufukuza kabisa umaskini nimeweza kuwekeza kwenye duka la nguo za kiume hapa DODDMA, linaitwa Mserereko Outfits. Bei zangu ni sawa na hamna. Nipo kwenye tasnia hii kwa miezi 7 sasa na progress naiona.

Nataka kukua wakuu, nataka kuuza jumla kwa bei sawa na za kkoo, kwa hapa dom nitawashika wafanya biashara wengi sana wa mavazi. Changamoto ni mtaji wakuu. Kwa sasa nina thamani ya around 7M+

Nimewahi kuweka chapisho hapa la kuomba connection ya watu wa kkoo ambao tunaweza ingia nao makubaliano wawe wananipa mzigo nasukuma tunalipana. Kuna mtu nilimpata bado tupo kwenye kuwasiliana zaidi kwa sasa na si biashara.

Narudi tena wakuu nahitaji sana msaada wenu wa connection za madon wa kkoo, nipate mzigo wa mkopo nianze kupush jumla. Nguo pendwa ni jeans na tshirts round, f6 na v neck. Kwa yeyote mwenye connection tusaidiane maisha jamani.

Kazi njema
 
I think pamoja na maombi yako ungeweka tangazo zaidi kuhusu duka lilipo, directions, bei za bidhaa zako, kapicha kidogo ya aina ya bidhaa zilizopo n.k.

Hii itasaidia hata kama mtu hana connection lakin anaweza kupita hapo kukuchangia kwenye manunuzi. Ni mawazo yangu.

NB. Hakikisha hauuzi maronyaronya kama ya yule jamaa anaitwa furedi
 
Daa safi sana kwa akili yako hii, although naangalia akili ya Mtanzania huyu huyu ninaye endelea kujifunza tabia yake je, atakupa connection au ile roho mbaya, kinyongo na kwa nini ufanikiwe ndivyo vitatawala!
 
Nimelichukua. Vitu genuine mkuu
 
Daa safi sana kwa akili yako hii, although naangalia akili ya Mtanzania huyu huyu ninaye endelea kujifunza tabia yake je, atakupa connection au ile roho mbaya, kinyongo na kwa nini ufanikiwe ndivyo vitatawala!.
Wapo watu wenye roho safi mkuu. Na ninaamini kabisa wapo. Wapo watu wanashusha mizigo mukubwa kutoka nje na kuna muda wanastragle kuiuza, mtu kama huyo ukimpata ni rahisi sana kufanya kazi. Kikubwa uaminifu tu
 
Ka ofic kangu mukuu, siuzi lonya kabisa. Na ikitokea nimeagiza ikaja lonya huwa naitudisha.
 
Watu wapo kaka ila sio kirahisi inabidi mpaka ufanye nao kazi kwa kiasi flani mjuane lakini ghafla bin vuu kukopesha ni kazi kaka
 
Wapo watu wenye roho safi mkuu. Na ninaamini kabisa wapo. Wapo watu wanashusha mizigo mukubwa kutoka nje na kuna muda wanastragle kuiuza, mtu kama huyo ukimpata ni rahisi sana kufanya kazi. Kikubwa uaminifu tu
Maboss wapo kaka Ukifika Kariakoo Ulizia Nondo kuna Zebedayo kuna Maiko Kuna Kimboli hao ni Maboss wakubwa ila Kukukopesha bila kuanza nao biashara mdogo mdogo ni kazi kidogo kwa Mfano huyo Nondo Kuna Braza Moja Hapa Tunduma Ni Mwanangu Juzi Kati Kakopa Mzigo Wa 20 million
 
Kuna suruali ipo lonya hapo kaka mstari wa nne kutoka juu upande wa kulia ni lonya unauza pei gani pia softjeans unauza jumla bei gani ili nipine range ya bei zako mkuu
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Hizo ndio connection kaka, najua lazima tufanye nao kazi hata mwaka kwanza kujenga mahusiano. Nampataje mkuu
 
Unapochukulia mzigo kwa sasa, ukijenga uaminifu watakupatia mzigo kwa mkopo.
Kwa mwanzoni unaweza kuanza nao hivi:-​
  • Unawatumia pesa kiasi fulani kwa kuwaamini ili wakufungie mzigo wakutumie​
  • Hakikisha mzigo uliopo aukai dukani mda mrefu; hakikisha ndani ya siku saba umeisha.​
  • Hakikisha angalau kila wiki unaagiza mzigo​
  • Kwa mazingira hayo, utakuwa umewatengenezea mazingira ya kukuamini​
  • Baada ya hapo; agiza mzigo kwa mali kauli na ndani ya siku saba unawapa pesa yao.​
  • Agiza zaidi na zaidi ili uweze kukua zaidi​
 
Kuna suruali ipo lonya hapo kaka mstari wa nne kutoka juu upande wa kulia ni lonya unauza pei gani pia softjeans unauza jumla bei gani ili nipine range ya bei zako mkuu
Acha lugha za kebehi kwa biashara za watu
Kama kweli mnunuzi mfuate dm
 
Acha lugha za kebehi kwa biashara za watu
Kama kweli mnunuzi mfuate dm
Broe sio kebehi mimi mwenyewe ni muuza nguo tena nauza lonya Ninauza Dg Dar 10000 mimi nauza 11000 bei ya jumla nauza suruali 13000 Dar Nanunua 12000 Nineuliza kuhusu bei za soft jeans ili nipime bei zake kadeti tunachukua 12800 dar bei ya jumla Tunduma tunauza 13500 hadi 14000 ko nataka nijue Range ya Bei Zake
 
Sometimes jifunze kuridhika, usijaze mali mpaka mteja akija dukani akose kumbe nguo ipo.
Weka duka safi kama unataka mzigo mkubwa weka stoo.
 
Boss bonge la idea, changamoto iliyopo ni kwamba kuna kijana anaitwa niko hapo wanyama hotel ndio anaenifungia mizigo yaani nikiagiza mzigo hata kama nachukua kwa watu watano tofauti yy ndio namtumiaga pesa wengine wote wanaleta mali kwake anawalkpa. Huyu huwa nananikopesha bando za jeans akiwa nazo, changamoto yake huwa hauzi nguo za juu.

Mfano tangu mwaka jana October alishusha track suits kwangu sio deal, sasa ivi ameshisha kadets kwangu sio deal. Ila bado ananifungia mizigo nokiagiza hata kama sichukui chochote kwake. Kijana mmoja smart sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…