Bado natafuta mantiki ya kujenga hili Daraja la Kigongo - Busisi kwa Tshs. Bilioni 700

Hakuna umuhimu wowote ule maana kibiashara Uganda haitegemei sana Tanzania kutokana na uhuni wa kodi. Yani ule ni upotevu wa fedha za umma
Elewa comment kabla huja reply, nimesema wanufaika ni Rwanda, Burundi na Congo DRC wanapotumia bandari ya Mombasa badala ya kupitia Kampala watakuwa wanapitia Mwanza.
 
Daahhh mawazo mengine bana hadi kero kwa kweli.
Jamaa anakera sana yaani ameliona daraja la Busisi pekee halina umuhimu kwa kuwa liko kanda ya ziwa ila hajaona madaraja yaliyojengwa sehemu nyingine kama daraja la Rufiji, daraja la Malagalasi, daraja la mto Kilombero, daraja la Nyerere na n.k.
 

..zaidi ya daraja kuna alternative gani nyingine?

..hebu tuelezee kidogo JIOGRAFIA ya eneo hilo na changamoto zake.
 
Elewa comment kabla huja reply, nimesema wanufaika ni Rwanda, Burundi na Congo DRC wanapotumia bandari ya Mombasa badala ya kupitia Kampala watakuwa wanapitia Mwanza.
Huyu jamaa haijui hiyo barabara, hii njia inaunganisha kenya na nchi za Rwanda Burundi na DRC.

Pili nahisi vilevile alikuwa anafikiri hili daraja ni kama la kigamboni kwa maana ya kuhudumia watu wa dar tu, sasa nahisi na hili alifikiri ni kwa ajili ya mza tu.

Kwanza anatakiwa ajue daraja hili zaidi ya km 30 kutoka jiji la mwanza.

Mabasi na malori kuelekea kagera, Geita, kigoma hii ndio njia yao.

Wanasema iongezwe Ferry nyingine tu ingetosha nafikiri atembelee eneo aache habari za kuambiwa.

Tatu, nahisi huyu ni moja ya wale watu ambao wakisikia mradi wowote mza wanataka kujenga hoja mza inapendelewa.
 
Cha kujiuliza kati ya Daraja la Kigamboni lenye urefu wa meter 680 lilojengwa billion 315TZS na Daraja la Busisi linalojengwa kwa billion 700 TZS lenye urefu wa meter 3200 Daraja lipi limejengwa kwa bei nafuu?
 
Ni kutupa fedha za maskini baharini. Bilioni 700 tungejenga barabara kilometer 700 kanda ya ziwa ingeunganishwa wilaya zote kwa barabara safi ya lami.
Acha upuuzi bilioni 700 ndiyo unaona pesa nyingi kwenye nchi kama Tanzania? Acha mawazo ya kimaskini, kwanza daraja limechelewa sana kujengwa lilitakiwa lijengwe miaka ya 60 kutokana na umuhimu wake kwa sababu linaunganisha zaidi ya nchi nne za Uganda,Congo DRC, Rwanda na Burundi. Magari yanayoenda nchi hizo huwa yanapita kwenye hicho kivuko cha Busisi.
 

Hizo ni baadhi ya ferry mbili kubwa zinazotoa huduma kwenye eneo la Kigongo- Busisi hapo kila ferry inabeba gari zaidi ya 35. Pamoja na ukubwa huo hata ukifika saa nane za usiku utakuta zinatoa huduma. Mv. Mwanza na Mv. Misungwi


Hiki ni kivuko kidogo kwenye eneo la Busisi kinaitwa Mv. Sengerema
 

Attachments

  • 1600286889841.png
    830.6 KB · Views: 1
..zaidi ya daraja kuna alternative gani nyingine?

..hebu tuelezee kidogo JIOGRAFIA ya eneo hilo na changamoto zake.
Alternative iliyokuwa bado hajatumika ni daraja pamoja na kuogelea (kupiga mbizi) sasa tumeona kuwa wengi hawajui kuogelea hivyo tumeamua kujenga daraja!
 
Chadema wanahisi kuwampinzani ni kupinga kila jambo zuri la serikali.
Chadema mnapokea ruzuku ya chama kila mwaka,kwa nini mmeshindwa kujenga hata ofisi kuu ya chama chenu.mnakalia kukosoa tu?View attachment 1570232
Wanapata ruzuku ya zaidi ya bilioni tatu kila mwaka lakini wameshindwa hata kupiga rangi makao makuu ya chama achilia mbali kujenga ofisi ya makao makuu ya chama.
 
Itakuwa pouwa sana, daraja likikamilika hizi ferry ziletwe eneo la Kamanga
 
Chadema acheni upuuzi wenu wakati wanajenga madaraja ya Mkapa, Kilombero, Nyerere, Malagalasi na n.k, watu wa kanda ya ziwa hawakulalamika lakini linapojengwa daraja la Busisi mnapiga kelele hii si sawa hata kidogo. Hamujui mateso waliyokuwa wanapata wakati wa kusubiri Ferry hasa wakati wakiwa na wagonjwa.
 
Yaani dereva tulie nae kapinda kinoma ,huku watumishi wanalia, wakulima ni shida ,wafanyabiashara wanajifia kwa pressure
 
Kwa watanzania ambao niwajamaa hawawezi kuelewa umuhimu wa muda.

Hakuna kitu huwa sipendi Kama kupoteza muda, muda ni mali.

Nikipiga hesabu ya muda na kwamba mwaka 2012 nilipita hapo nikapoteza muda naunga mkono maeneo yote yenye shida Hiyo yajengwe madaraja kama hayo.

Sent from my Infinix X603 using JamiiForums mobile app
 
So ndio kusema tukimchagua Lissu hamtajenga hilo daraja,at least watu wake Mwanza na kanda ya ziwa mjionee,maendeleo yakiletwa huko yanapingwa!

Ni nini inakuja akilini baada ya kusoma hii thread,kazi kwenu.
 
Kweli ujinga ni mzigo, kwa hyo umeambiwa wagonjwa na watu wanaovuka hapo wanatoka Sengerema tu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…