Tanzania ukiwa kiongozi na ukataka kumfurahisha kila mtu, nchi haiendi; wapingaji kama wewe wapo tu, na wengine hupinga kwa sababu lilijengwa wakati wa Magufuli, lingejengwa wakati wa Kikwete au Samia huenda wasigentoa lawama hizo.
Inaonekana unaangalia daraja like kwa lenzi ndogo inayoona kuunganishwa kwa Busisi na Kigongo tu. Hujui kuwa linahudumia pia mikoa ya Kagera, Geita, na nchi jirani za Uganda na Rwanda. Kuna siku hapa mama Tibaijuka alilalamika mkoa wa Kagera kuwa wa mwisho kimaendeleo na sababu yake ni hiyo ya usafiri baina ya mkoa wa Kagera na Mwanza kuwa magumu sana. Meli zimepunguza tatizo hilo kidogo lakini huwezi kulinganisha na huduma ya barabara. Matumizi ya feri hayawezi kutatua changamoto za usafiri eneo hilo, mpaka sasa hivi kuna feri pale Bisisi-Kigongo, na Kamanga lakini hazitoshelezi; kwanza zinafanya kazi mchana tu. Ukifika hapo saa 12 jioni, itabidi ulale hapo hadi kesho yake.
Daraja lina urefu wa zaidi km 3 likiwa ni refu kuliko yote Tanzania, kwa hiyo gharama ya $300m ni wastani wa $100m/km ambayo ni chini ya gharama iliyotumika Tanzanite Bridge ($121/0.63) kwa kila km.