Bado sijaona zile fujo za Patrik Viera Vs Roy Keane

bryan2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,323
Reaction score
4,679
Bado pale Epl sijaona zile fujo za Viungo wa kati kama zile za Viera wa Arsenal na Keane wa Man utd hawa majamaa kila wakutano ulikua n mpira wa shoka haswa eneo la kati.

Kati ya mmoja wao kula umeme ilikua ni kitu cha kawaida hawa viungo wa sasa wanacheza Soft football sana hawa mafundi walikua wamekamilika kila idara za kuitwa viungo wakabaji.

Mchezo wa kesho zitakapokutana hizi timu mbili bado nategemea eneo la kiungo liamue matokeo ya hii game atakayewin eneo la kati ndo atakayeshinda.
 
 
Ila zakina poul ince na wakina cantona umeziona!!!
 
Siku hizi mechi za Arsenal na Manutd ni mechi za kawaida sana. Ndio maana zinachezwa usiku. Enzi zile mechi hizi lazima ichezwe mchana kweupe. England mara nyingi mechi ambazo ni kali na zina upinzani mkali hadi kwa mashabiki huchezwa mchana kweupee ili polisi waweze ona matukio vizuri.
Enzi hizo matukio yalikuwa ni ON na OFF the pitch.
 
Endelea kuwasubiri kila zama zake
 
Endelea kuwasubiri kila zama zake
Kwa kifupi nini tatizo tena wasitokee wachezaji wa kariba ile tunaona leo viungo wakabaji wenye mapafu ya mbwa hakuna tena,Makelele,Ballack,Viera,Roy keane tunaona viungo wakicheza mpira laini sana,ozil,Xhaka,Ramsey,bora hata Ngolo Kante.
 
Ng'olo Kante....ndio namba sita pekee isiyobahatisha.
 
Unataka uone mpira au fujo na ngumi?

Ulishawahi ona tuzo ya utukutu?
 
Unataka uone mpira au fujo na ngumi?

Ulishawahi ona tuzo ya utukutu?
Umemshuhudia Gennaro gatuso akicheza wewe?wale walikua ni viungo wanaojua kutimiza wajibu wao na sio fujo wala ngumi.
Muulize Christiano Ronaldo Man utd vs Ac milan pale San Siro kama alipigwa ngumi.
 
hatariiiihatariiiii duu gattuso yaani christian ronaldo baada ya kuona ubaunsa wa gattuso ilibidi atembee tu uwanjani maana hawezi kumiliki wala kupiga mbele ya gwiji gatu
 
hatariiiihatariiiii duu gattuso yaani christian ronaldo baada ya kuona ubaunsa wa gattuso ilibidi atembee tu uwanjani maana hawezi kumiliki wala kupiga mbele ya gwiji gatu
Akienda pembeni anakutana na Cafu, Rooney na Stam.
 
usitegemee koqwelin kuleta fujo za viera ndugu
 
Siku hizi kuna teknolojia kwahiyo hata usiku wataona tu
 
usitegemee koqwelin kuleta fujo za viera ndugu
Na ile Arsenal ya Viera ilikua chini ya huyu mzee wetu Wenger ila wale viungo walikua makini na kuitambua kazi yao tangu atoke Alex Song pale hakuna kiungo namba 6 makini Arsenal.
 
Siku hizi kuna teknolojia kwahiyo hata usiku wataona tu
Kuna mechi zinachezwa mchana kutokana na aina ya mashabiki kama Liverpool na everton game inapigwa mchana ili kuzuia fujo za mashabiki maana asilimia kubwa ya mashabiki ni chapombe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…