Bado Trilioni 3 Tu TRA (Tzn) Kuipita KRA (Ken) Makusanyo ya Kodi. Kishindo Cha Tanzania ya Samia Kitapeleka vilio Kwenye Uchaguzi wao 2027

Mama akifikisha SGR Mwanza na Kigoma ikaanza kubeba mizigo ya nchi jirani Kenya wamekwisha!!

Sijui anakwama wapi bimkubwa maana hiyo ndio legacy yake itayomfanya kila anapopita raia wampe maua yake milele na milele.
 
Mama akifikisha SGR Mwanza na Kigoma ikaanza kubeba mizigo ya nchi jirani Kenya wamekwisha!! Sijui anakwama wapi bimkubwa
Watakwisha hata kabla ya SGR.By 2030 SGR ndio itakuwa imekamilika.

Sikuiweka kwenye list Kwa sababu Kwa Sasa Haina faida kiuchumi ila inatumia ruzuku kujiendesha.
 
Watakwisha hata kabla ya SGR.By 2030 SGR ndio itakuwa imekamilika.

Sikuiweka kwenye list Kwa sababu Kwa Sasa Haina faida kiuchumi ila inatumia ruzuku kujiendesha.
Kila kitu ni mipango and political will, Bimkubwa akiamua wajenge SGR usiku na mchana kwa kuona faida yake labda 2027 inaweza kukamilika, ule mradi utainyanyua tz hadi uchumi wa juu sana na utarudisha pesa yote fasta. Shida ni kuwa kuna wanaopinga wenye malori na mabasi!!
 
Uchumi kiserekali unakuwa, lakini mtu mmoja mmoja unadidimia, except akina ZAKAYO, WATOZA USHURU KWAO ALHAMDULILAH.
 
VAT mkitukuta tunafikiri wakati nyie mliofaulu Darasani mpo tuchapeni viboko - Kodi kwa maendeleo ya Taifa pamoja na Mshindano na nchi nyingine
 
Nimesoma uzunguni nchi tajiri kule hakunaga ufaulu wa hivyo A zote darasa zima, kule pepa ngumu huoni pa kutokea, ndo maana Africa ni maskini milele
Ndio Tunawaachia nchi yao ni ya wote kufaulu ndani ya Nchi Ya Mabadiliko ya kila kituuuuuuu....

Yaani hakina cha Maana kabisa Mtaani na shuleni kwa mujibu wake yule mwanazuoni wa Africa
 
Naona hapa najirudia kama Santuri tu ? Na uelewa wako inaonekana ni mfupi sana..., Ni hivi narudia tena kwa mara nyingine.., Makusanyo / Makamuzi yameongezeka maradufu na hayaendani sambamba na Huduma zinazotolewa..., Ukizingatia Serikali hii ya Madalali ambayo imeshajijengea kwamba kila kitu hawawezi tulete wengine wanfanye (hivyo kupunguza hata matumizi ambayo wangetumia otherwise) kwahio in short hakuna value for money...

Pili huwezi kujisifia tumiradi twa maji wakati misaada na mikopo lukuki inakuja kila mwaka kwa ajili ya maji..., sasa iwapo huko Jangwani watu wanapata maji na hakuna ma cheerleaders wanaosifia hilo (wewe kuleta hapa hio kama justification ya makamuzi) nakuona kama Punguani.

Tatu kwa kuona kwamba Corruption haiwezi kuisha kwa taifa / bara ambalo curroption ndio imetufanya ombaomba nakubaliana na wanaosema kwamba yule anayeleta na aliyeleta tatizo huwezi kumtegemea kumaliza tatizo hilo...

Mwisho kabisa hii Notion kwamba lazima uwe na Kodi ya Mapato ili mambo yaende kwenye nchi yenye vyanzo vya kuwaga ndio mtaji wa wanasiasa wanaotumia kuwalaghai watu wenye mawazo kama yako kuridhika na mediocrity...
 
Ni lini mlikuwa hamkamuliwi? Kama haiendani na Huduma lipa Kodi zaidi Ili upate stahiki hakuna Cha bure.Wengine waliopunguza matumizi wakafanikiwa ni kina nani hao na waliopunguza nini na wakafanikiwa kipi.?

Mikopo sio Msaada inalipwa na Kodi na ni lazima ,Nchi zote zilizoendelea Zima madeni mara dufu ,Tanzania hatuna Hilo deni mara dufu.Mtu akikupa Msaada pokea na tumia.ila.Tanzania inaenda bila Msaada , kwenye Bajeti hiyo Msaada hazifiki hata Trilioni 4 kati ya Bajeti ya Trilioni 44.Mwisho Taja Nchi ambazo Viongozi hawasifiwi.

Kodi lazima hapa Duniani kama hutaki kulipa Kodi hama sayari maana hakuna utakakoenda usilipe Kodi.

Kazi ya kusambaza maji inaendelea hapa Ruvuma ,biloni 146 zimemwagwa 👇👇

View: https://www.instagram.com/p/DFM38TlM-s5/?igsh=MXI0YzN1em4zYWZoNw==
 
Pesa inahitajika maeneo mengine kuliko Sgr tuu.

Hatuwezi ku paralyse uchumi kama awamu ya 5 eti kwingine kusimame kisa Sgr na bwawa,hiyo haiwezi jirudia ni hasara Kwa ustawi na ukuaji wa Uchumi.

Sgr itajengwa kadiri ya hela zinavyopatikana no rash.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…