Nangu Nyau
JF-Expert Member
- Jul 1, 2022
- 5,015
- 14,139
Mbona ndivyo ilivyo? Wewe sema ukuaji wa Uchumi Kwa Sasa Bado sio mkubwa sana kuwa na far reaching multiplayer effects ,ipo Kwa kiasi Cha wastani japo Huduma za Umma zimeimarika sana hasa Afya ,Elimu na maji.
Sisi wote ni watanzania jamaa yangu, tunatembea hii Tanzania kila kona, hizo huduma unazosema zimeimarika mbona hatuzioni, sio tu mikoani hata hapo Dar es salaam.
Kama Dar es salaam Kuna malalamiko ya ukosefu wa maji itakuaje huko kazuramimba? , hivi unajua hapo Morogoro tu na Pwani bado watu wanakunywa maji ya miferejini na kwenye mito?
Ukiangalia matokeo ya jana ya Form four bado unakuta shule Moja Ina wahitimu wa form four tu zaidi ya 400.
Malalamiko ya maslahi ya walimu Kila siku kelele, huo ubora wa elimu uko wapi sasa?
Hizo huduma za Afya unazosema zimeimarika, mbona hapa juzi Kuna viongozi kadhaa wakubwa wamefia India na sio Mloganzila?
Ulishawahi kwenda Mloganzila au Muhimbili ukajionea msongamano?
Jiji la Dar es salaam hospitali zoote referral wanapeleka Muhimbili na Mloganzila hakuna option nyingine?