Kwahio Dalali Kafulila kila siku anavyoleta hizi hadithi za PPPs ni Hadithi tu ? Au zitaanza lini na Kodi itapungua lini ?; Na kwahio PPPs inafaa kwenye Mabweni na UMEME wetu na TEMESA kwanini huku ambapo kuna uhitaji wasifanye hao ? Au PPPs haikubaliki kwenye Barabara ?
Sasa bila kujua percent imetoka wapi na ngapi unawezaje kusema Matumizi yako yametumika vizuri wakati hayo mengine ni kwa Mikopo ambayo ni wajukuu zako ndio watalipa ? Hivi naongea na mtu mwenye ufahamu na fikra au ROBOT / AI ambayo inafanya ku copy na kupaste bila kushirikisha reasoning yoyote ?
Na unaongelea maji bila aibu wakati kuna watu sehemu kama Mwanza ziwa wanaliona lile pale na bado mabomba yameota kutu na maji kwao kuyaona ni kama miracle ?!!! Na unajua misaada mingapi na pesa ngapi nchi hii inapokea kwenda kwenye sekta ya Maji ?
Kwa ufupi tu ngoja nifanye simplification ili hata wewe uweze kuelewa...; Leo mtu ambaye anatoa kingi kuliko hapo kabla (kila akinunua anakatwa kodi, akituma muamala anakatwa, akiongea na simu anakatwa, akiingia income anakatwa) Mtu huyu bado kila huduma anayotapa bado analipia (Makazi, Mavazi na hata Elimu) ambapo hawa walamba asali waliopo hapo juu waliweza kupata hivyo kama huduma (Elimu na Afya) wakati makusanyo yalikuwa madogo kuliko haya na wala kulikuwa hakuna teknolojia ya ukusanyaji wenye ufanisi kama huu....
Na kwa kukuongezea kama Corruption ikiondoka Tanzania na Afrika kwa ujumla haitahitaji hata senti moja kutoka nje..., na mpaka dakika hii na hata kabla wealthy has been moving from Africa to Developed Countries...
View attachment 3212475