Bado unayo nafasi

Story nzima ya Bustsni ya Edeni ni lugha ya picha..Mungu aliumba primary being ambao ndio hao Adam and Co baadae akatupa uwezo wa kuendeleza uumbaji kwa njia ya uzazi. Technically ngono si ajili ya kupata raha ni kuendeleza uumbaji wa Mungu.

Technically ngono si ajili ya kupata raha? Ngono ni kwa ajili ya kupata raha na kuzaliana, sio uumbaji. God created Adam, that's all he did.
 
Kwahiyo unaamini kwamba Mungu hayupo?

Kila alichokiumba Mungu na tazama aliona chafaa.

Hayo yote uliyosema yanatokana na anguko la mwanadamu.
Go and read Genesis chapter three..Go through the whole chapter..
It's all about "The fall of man"

Hilo anguko la mwanadamu ndio kalizungumzia Mkuu kwenye hoja yake kuwa, Kama Mungu alijua kuwa Adam ataanguka na atakayeangushwa na Shetani..!?Kwanini aliruhusu hilo litokee kama yeye yu Mjuzi na mwenye upendo wa pekee kwa Kiumbe chake Adam??
Sikatai kuwa Mungu yupo, naamini mnoo na naamini sana yupo hata leo nimeshuhudia vile ameniwezesha kuamka mzima wa Afya.. Swali langu li juu ya Wema wake Mungu wetu..! Mbona yu mwema kwa baadhi ya watu na si kwa wote ?? Kuna watu wanapitia magumu sana na wakati mwingine unaweza sema si bora Mungu aichukue tu hiyo roho yake ??
Kuna Atheist mmoja aliweza kusema, “I do not question the existence of God, but his Goodness “ .... Mungu wetu anatupenda ndio ila ila uzuri kwa kila kiumbe chake ndio bado sijawahi kuuthibitisha kwa kweli.

Good morning babe @Sainte Anne
 
Mara nyingi mtu anapopoteza hope na kuona hana alternative nyingine ndio huwa anajikuta amepata msaada bila hata yeye kufahamu umetoka wapi!

Suala la kuamini Ukuu wa Mungu au Wema wa Mungu ni vile wewe umetendewa...! Kuna mikasa mingine inatokeaga kwa watu unabaki na maswali tu na hata majibu yake ukiwafuata wasomaji wa Biblia watakuambia “Bwana anatenda kwa wakati wake, muda wa Mungu ndio sahihi zaidi.!”
Swali linakuja, kwanini kuna watu wanafariki wanaacha familia ambayo inakosa msaada kabisa na wakati mwingine watoto wanapata Tabu mpaka unaweza kuuliza kwanini waliletwa dunia..?? Ili wateseke ? Kwanini hawa watoto wanateseka hivyo, kosa lao li wapi ..!?? Mimi leo nimeamka salama Namshukuru, ila leo hii hii kuna mtu mahali fulani kafa na wakati mwingine ameacha familia ambayo ukiangakia kabisa itapitia kipindi kigumu mnoooo [emoji24]
Naomba niishie hapo huenda nikajikuta nimeandika maneno mengine watu wakaniona labda mie nampinga Mungu ili hali hata sina uwezo kabisa wa kupinga kazi zake ila maswali ninayo mengi juu ya Wema wa Mungu.
Ila Namshukuru kwa kuniamsha salama[emoji24][emoji24][emoji24]
 
Tatizo ni pale unapotaka Mungu afanye vile unavyotaka wewe.
Kila alichokiumba Mungu na tazama aliona ya kwamba ki chema.

Alimuumba mwanadamu,akampa uhuru,kiburi cha mwanadamu ndicho kikichomponza.
Unauliza kwanini kama alijua mbona alimuumba shetani???
Jibu ni kwamba ujinga wetu ndo uliotuponza,,,if things fall apart usitafute wa kumlaumu,,jilaumu mwenyewe..
Msianze kutafuta mumpangia Mungu afanye vile mnavyotaka..
Mawazo yake si kama mawazo ya mwanadamu.

Hutaki kumuamini acha!
Hakuna anayekulazimisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…