Bado Yanga wana kikosi kizuri zaidi ya Simba

kwisha

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2021
Posts
1,779
Reaction score
4,982
Watu wengi wanaweza kuona kikosi cha Yanga ni cha kawaida kutokana na sajili za Simba lakini kwangu mimi bado Yanga wana kikosi kikubwa zaidi ya Simba hasa hasa washambuliaji wa Yanga.

Kipindi cha nyuma niliwahi kusema ni marufuku kucheza na Yanga huku ukiwa unacheza kwa kuwashambulia kwa Wingi zaidi utakuwa unajitafutia matatizo ya kifo cha kujitakia.

Yanga ni wabaya zaidi ukiwapa nafasi ya kukimbia na mpira iwe katikati au pembezoni mwa uwanja
Maana wana washambuliaji wenye kasi zaidi na nguvu kuliko timu yeyote nchini.

Na wakienda na mpira wao huu kimataifa hakika yanga bingwa full stop.
 
Kipindi cha nyuma niliwahi kusema ni marufuku kucheza na Yanga huku ukiwa unacheza kwa kuwashambulia kwa Wingi zaidi utakuwa unajitafutia matatizo ya kifo cha kujitakia

Aisee! Ni kweli hilo? Mbona goli la Kibu dhidi ya Yanga kulikuwa na washambuliaji wanne wa Simba dhidi ya walinzi wawili wa Yanga, ina maana Simba walikiuka mwiko huo kwa kuishambulia Yanga?
 
Yanga unaowazungumzia ndio wale waliofungwa mbili bila na Simba au Kuna Yanga wengine
Yanga hawakuitaka Ile mechi...walikuwa wanajiandaa na mechi za Caf.....na walikuwa wanauona ubingwa wa ligi ya NBC,Simba ilikuwa pungufu point 8.....wachezaji walikuwa wanawaza nusu fainali ilikuwa.
 
Hakuna kitu kama hicho , Simba na Yanga zote zilikuwa na mechi ngumu mbele yao hivyo aliyefungwa alizidiwa uwezo tu mkubali kuliko kujitutumua eti mlimwachia Simba
 
Kwanini Yanga kwenye champion league alicheza mechi mbili tu? Simba ambaye alikuwa na kikosi dhaifu amecheza champion league mpaka robo fainali na sasa anacheza Supercup?
Yanga ambayo imecheza shirikisho fainali kwanini kwenye supercup haipo?
Icho unachokisema kitathibitishwa msimu huu kama aliyecheza mechi 2 alikuwa dhaifu ama lah! Mwenzako alikutana na Al hilal na wewe ukaenda kukutana na ihefu wa angola na wakati huo huo muunganiko ulikuwa bado aujaklick ndani ya yanga nafikiri nimekujibu!
 
Yanga hawakuitaka Ile mechi...walikuwa wanajiandaa na mechi za Caf.....na walikuwa wanauona ubingwa wa ligi ya NBC,Simba ilikuwa pungufu point 8.....wachezaji walikuwa wanawaza nusu fainali ilikuwa.
utetezi was kitoto lakini utoto unakusumbua hizi mechi ni zaidi ya unavyozijua I;a kwa sababu umeanza ushabiki juzi ndio maana ukajibu hivyo.
 
Icho unachokisema kitathibitishwa msimu huu kama aliyecheza mechi 2 alikuwa dhaifu ama lah! Mwenzako alikutana na Al hilal na wewe ukaenda kukutana na ihefu wa angola na wakati huo huo muunganiko ulikuwa bado aujaklick ndani ya yanga nafikiri nimekujibu!
Kwa hiyo Simba ilikuwa na muunganiko kuliko Yanga ila Yanga akamfunga Simba kwenye ngao kisha Yanga akafungwa na Al Hilal kisa hana muunganiko hivi ninyi mnatafakari kwa kutumia vichwa vyenu vizuri kweli? [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwanini Yanga kwenye champion league alicheza mechi mbili tu? Simba ambaye alikuwa na kikosi dhaifu amecheza champion league mpaka robo fainali na sasa anacheza Supercup?
Yanga ambayo imecheza shirikisho fainali kwanini kwenye supercup haipo?

Kabisa kabisa. Kwa hoja ya super cup hata TP Mazembe nae alicheza robo fainali kama Simba kwenye champion league ndio maana supercup yupo.
 
Watu wengi wanaweza kuona kikosi cha Yanga ni cha kawaida kutokana na sajili za Simba lakini kwangu mimi bado Yanga wana kikosi kikubwa zaidi ya Simba hasa hasa washambuliaji wa Yanga.

Kipindi cha nyuma niliwahi kusema ni marufuku kucheza na Yanga huku ukiwa unacheza kwa kuwashambulia kwa Wingi zaidi utakuwa unajitafutia matatizo ya kifo cha kujitakia

Yanga ni wabaya zaidi ukiwapa nafasi ya kukimbia na mpira iwe katikati au pembezoni mwa uwanja
Maana wana washambuliaji wenye kasi zaidi na nguvu kuliko timu yeyote nchini

Na wakienda na mpira wao huu kimataifa hakika yanga bingwa full stop
Hongera Kwa kujifariji
 
Icho unachokisema kitathibitishwa msimu huu kama aliyecheza mechi 2 alikuwa dhaifu ama lah! Mwenzako alikutana na Al hilal na wewe ukaenda kukutana na ihefu wa angola na wakati huo huo muunganiko ulikuwa bado aujaklick ndani ya yanga nafikiri nimekujibu!
Ukiona umepangiwa timu ngumu jua wewe ndo dhaifu. Kwa hiyo utopolo ni luza kama luza wengine.
 
Back
Top Bottom