Mnakumbuka embe ng'ong'o zile ambazo kokwa lake lina miiba, mafenesi, madansi ( ile jamii ya machungwa makubwa ka kichwa cha mtoto). Mawazo Potofu tuliyojijengea ni kuwa sasa hivi kula hayo ni ushamba bwana watu wanywa juice ya pakiti, burger, ice cream etc.
It is obvious huwezi kuwa kwenye benzi ukaanza kula mabungo mafenesi and other traditional fruits.
Jiulize nani anakula miwa siku hizi, viazi vya kuchoma, ndizi za kuchoma ( wale wanaoenda bar wanabahati kupata hizo), Kisamvu, mboga za majani ya maharagwe au kunde. Kuna togwa, ufuta, kashata hakuna nutritionist afanye tafrija ya vyakula asili vya kitanzania.