Bado yapo haya!?

Bado yapo haya!?

Mnakumbuka embe ng'ong'o zile ambazo kokwa lake lina miiba, mafenesi, madansi ( ile jamii ya machungwa makubwa ka kichwa cha mtoto). Mawazo Potofu tuliyojijengea ni kuwa sasa hivi kula hayo ni ushamba bwana watu wanywa juice ya pakiti, burger, ice cream etc.

It is obvious huwezi kuwa kwenye benzi ukaanza kula mabungo mafenesi and other traditional fruits.

Jiulize nani anakula miwa siku hizi, viazi vya kuchoma, ndizi za kuchoma ( wale wanaoenda bar wanabahati kupata hizo), Kisamvu, mboga za majani ya maharagwe au kunde. Kuna togwa, ufuta, kashata hakuna nutritionist afanye tafrija ya vyakula asili vya kitanzania.

Ngambongali je unakula songwa, mangubwisi na ndilolo? nimefikiria you should know what ndilolo is given your name?
 
Labda kama hujafika kyela mkuu, nimeogopa kutaja matunda ya kikwetu kwa kuogopa ukabila, kwa kiswahili ndilolo ni zeituni au?

Kuna matunda yanaitwa fulu
 
It is obvious huwezi kuwa kwenye benzi ukaanza kula mabungo mafenesi and other traditional fruits.
Huu nao utumwa sasa, gari umeinunua wewe halafu bado inakupangia masharti ya nini ule au husile ukiwa ndani yake?
 
juice ya mabungo asikwambie mtu..........nyumbani kwangu never miss hiyo kitu.
 
Labda kama hujafika kyela mkuu, nimeogopa kutaja matunda ya kikwetu kwa kuogopa ukabila, kwa kiswahili ndilolo ni zeituni au?

Kuna matunda yanaitwa fulu

Hapana ndilolo kwa kiswahili ni Mafura fruits, zeituni kwa kiingereza ni Olives. Kwa lugha kilatin inayotumika sana kwenye masomo ya biology, mafura ni Trichilia Emetica.
 
X-Paster na WanaJF wenzangu, iwapo zeituni/mizeutuni inaitwa olives, je tunda lifuatalo linaitwa nini kwa Kiswahili?:

220px-Persimon.jpg
au
220px-Hachiya1.jpg

Thread reference: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...iumbe-hai-wadudu-wanyama-ndege-mimea-n-k.html
 
Labda kama hujafika kyela mkuu, nimeogopa kutaja matunda ya kikwetu kwa kuogopa ukabila, kwa kiswahili ndilolo ni zeituni au?

Kuna matunda yanaitwa fulu
Taja tu jina kwa lugha yoyote mkuu, hakuna cha ukabila wala nini, si aina zote za vyakula zina majina ya Kiswahili au Kiingereza. Vingine hata majina ya Kilatini inabidi kulazimisha tu!!

Mnakumbuka embe ng'ong'o zile ambazo kokwa lake lina miiba, mafenesi, madansi ( ile jamii ya machungwa makubwa ka kichwa cha mtoto). Mawazo Potofu tuliyojijengea ni kuwa sasa hivi kula hayo ni ushamba bwana watu wanywa juice ya pakiti, burger, ice cream etc.

It is obvious huwezi kuwa kwenye benzi ukaanza kula mabungo mafenesi and other traditional fruits.

Jiulize nani anakula miwa siku hizi, viazi vya kuchoma, ndizi za kuchoma ( wale wanaoenda bar wanabahati kupata hizo), Kisamvu, mboga za majani ya maharagwe au kunde. Kuna togwa, ufuta, kashata hakuna nutritionist afanye tafrija ya vyakula asili vya kitanzania.

Ngambo, sentensi yako jinsi ulivyoiweka hapo imekaa kiutata, kumbe unaelezea tu tabia za watu na si wewe unayefanya hivyo.
 
ubuyu, misasasti, matowo ( mitowo) mbula, mikusu, zambarau na misada.

Oh my childhood, I used to live in Kuboma then, every time I went to aga khan hospital I will go by soko la zamani and buy me some fulu ( mifudu) or misaada.
Na hujala peaches kama hujala dabaga peacheas
 
Taja tu jina kwa lugha yoyote mkuu, hakuna cha ukabila wala nini, si aina zote za vyakula zina majina ya Kiswahili au Kiingereza. Vingine hata majina ya Kilatini inabidi kulazimisha tu!!

Asante mkuu ngoja nikumbuke majina mengine ya matunda ya zamani,

Ngambo, sentensi yako jinsi ulivyoiweka hapo imekaa kiutata, kumbe unaelezea tu tabia za watu na si wewe unayefanya hivyo.

Benzi nitapata wapi mie, naelezea tabia za watu nani umemuona kwenye Benzi anakula mabungo, kama anafanya hivyo ni dereva na bosi wake akimuona ajira iko hatarini.
 
Huu nao utumwa sasa, gari umeinunua wewe halafu bado inakupangia masharti ya nini ule au husile ukiwa ndani yake?

Sio utumwa mokoyo, kuna vitu vinaemba sambambana hali fulani. Umewahi kuona mtu na Benzi yake anagida bia uswazi? Kama wapo ni wachache
 
Arooo
umenikumbusha enzi za kutumia manati na kuwinda joroe

makamilwa . jili ni tunda pori -fimbo ya mkamilwa ilikuwa na sifa ya kutokavunjika. walimu wakali enzi zile au mtoto mtukutu lazima upewe corpoal punishment ya mkamilwa

Mazambarau= matunda matamu ila miti yake ndo ilikuwa inaongoza kufanya watoto wa kiume wa primary ufungwe pop kwa sana sababu ilikuwa inateleza na tunadondoka

Mapera= Haya sifa yake unajua ukienda haja kubwa mbegu zinatoka live. wataalamu wa biolojia sijui wanaitaje huu msambazo wa mbegu.

Matope tope- Jamii ya mastafeli na mafenesi . hayana utamuuuuuu sana kama mastafeli . yenyewe ladha yake waweza kusema ni flat lakini ni mazuri

Nina hakika baadhi ya mataunda yako kwenye extinction. Inabidi kuwepo na porgram maalum ya kuyapreserve japo kwa maeneo machache.
 
ubuyu, misasasti, matowo ( mitowo) mbula, mikusu, zambarau na misada.

Oh my childhood, I used to live in Kuboma then, every time I went to aga khan hospital I will go by soko la zamani and buy me some fulu ( mifudu) or misaada.
Na hujala peaches kama hujala dabaga peacheas
misasasti-kama inalevya vile
mitowo-big G za kinyalu
mikusu-msitu wa mwatebela
mifudu-hii kitu sijaiona long time
 
Asanteni wadau!

Embe na pilipili ni moja ya mambo matamu sana tuliyopitia wengi wetu bila kusahau hogo na pili pili aaaaaaaaaaah we acha tu!
 
Lunanilo weye kweli mnyalu hivi sasa watoto wetu wanarundikiwa zile takataka toka Karachi na Kenya!
 
du kweli,umenikumbusha dada yangu alipokuwa mjamzito alikuwa ananituma mara nane mpaka kumi kwa siku gengeni
 
kuna ile mizizi inayopatikana sehemu kame kiasi jamii ya viazi fulani (ng'oti) we acha tu. mmenikumbusha mbali sana wakuu!!.
 
Kwa ukweli sidhani, hata kama yapo nafikiri hayauzwi tena mashuleni na mitaani. Si unajua mambo ya kiumagharibi yameharibu watoto wetu sidhani kama ukiwapa haya maembe wanaweza kuyala!
 
Arooo
umenikumbusha enzi za kutumia manati na kuwinda joroe

makamilwa . jili ni tunda pori -fimbo ya mkamilwa ilikuwa na sifa ya kutokavunjika. walimu wakali enzi zile au mtoto mtukutu lazima upewe corpoal punishment ya mkamilwa

Mazambarau= matunda matamu ila miti yake ndo ilikuwa inaongoza kufanya watoto wa kiume wa primary ufungwe pop kwa sana sababu ilikuwa inateleza na tunadondoka

Mapera= Haya sifa yake unajua ukienda haja kubwa mbegu zinatoka live. wataalamu wa biolojia sijui wanaitaje huu msambazo wa mbegu.

Matope tope- Jamii ya mastafeli na mafenesi . hayana utamuuuuuu sana kama mastafeli . yenyewe ladha yake waweza kusema ni flat lakini ni mazuri

Nina hakika baadhi ya mataunda yako kwenye extinction. Inabidi kuwepo na porgram maalum ya kuyapreserve japo kwa maeneo machache.

Mtazamaji umusahau MAKUNGU!!!!
 
Back
Top Bottom