Bado yapo haya!?

Eeeee bana! Nimekumbushwa mbali wakuuu.Nimevikumbuka viazi vya kukaanga na mafuta ya mawese na kuvila na chumvi! Duh! Maisha yale yalikuwa mazuri we acha.
 
kuna ile mizizi inayopatikana sehemu kame kiasi jamii ya viazi fulani (ng'oti) we acha tu. mmenikumbusha mbali sana wakuu!!.


Kule kwa mama yangu Ilembula kuna kitu kama hiyo inaitwa ng'ing'i
 
sasa hizi ndo afya kwa mwanadamu mwenye akili timamu
jamani mie haijalishi niko wapi,au gari gani au uboss gani,nikipata tu mwanwane najiachia fulu sina noma wala nn!!kwanini nikonee haya kitu kilichonifanya niwe na afya hivi.
je,mnafanya nini kuhamasisha familia zenu kuwa na vitu vya asili???mf kupanda miti ya matunda asili au kununua sokoni,mapera,mizeituni,parachichi,mifudu,embe ng'ong'o,fenesi nk au mboga za majani lol
sio watoto wa soseji na pizza ovyo kabisa
 
hahahah KABAZI
kweli kabisa kwa watoto walikulia mkoa wa mwanza enzi zile watakumbuka kulikuwa na mkungu karibu na jengo ya halmashuri ya manispaaa wakati ule. Vijana walikuwa wanatumia mashoto walikuwa wana shabaa kwenye mashindano ya kuangua haya matunda yote. sijui kisayansi kuna sababu..
 
Matobolwa (viazi vitamu vimekaushwa) wapi hii kitu..nikifika tabora lazima nitafute...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…