Bagamoyo Day Trip: Kwa Wakazi Wa Dar & Pwani

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
26,961
Reaction score
77,890
Poleni kwa hustling and bustling za mjini Dar.

Kuna hii "day trip" ya kwenda Bagamoyo unaweza kwenda na kujifunza vitu mbalimbali. Sio mbali sana, ni kilometa 70 kasoro kutokea Ubungo, na unaweza kwenda kwa usafiri wako (karibia masaa mawili kutokea Ubungo) au ukaenda kwa usafiri wa umma (magari ya kuunga ila jumla nauli haifiki elfu 5 hadi unafika).

Bagamoyo ni moja ya mji wa kihistoria uliopo Mkoa wa Pwani, ambako utajifunza mengi sana kuhusu utumwa, dini ya kikristo, ukoroni, maisha ya kale n.k



Wakazi wa Bagamoyo wanajishughulisha sana sana na biashara ya uvuvi na uuzaji wa samaki kutoka Bahari ya Hindi.



Wapo wachache wanajishughulisha na mambo ya utalii (mfano kutembeza wageni & arts), uvunaji wa chumvi (kwa evaporation), kilimo cha mazao na biashara ndogo ndogo.

1. Kanisa la Kale
Hapa utakutana na kanisa la kwanza kabisa Tanzania. Ambalo ndani yake utajifunza historia nyingi sana. Pia kuna jumba la makumbusho ya kale pembeni yake. Utajifunza mengi pia. Kiingilio kanisani ni Bure ila jumba la makumbusho ni Elfu 2. Hafu nje kuna vijana wa kukutembeza utampa tip ata elfu 5.



2. Soko la Samaki
Kuna soko kubwa la Samaki ambapo utakutana na wauzaji na wanunuzi mbalimbali. Kama unaweza kununua itakua poa tu.


3. Ngome ya Wajerumani
Ni sehemu ambayo Wajerumani waliitumia kama base yao ya kijeshi miaka ya 1880s. Hapa ukiwa na mwenyeji oana mbwembwe atatianutapenda.



4. Vyuo mbalimbali.
Kama unaweza utavisit vyuo kama SAUT (Marian University College), Chuo cha Sanaa, Branch ya MUHAS, Ifakara Health Institute, Kaole Agriculture Inst etc. Unaweza ulizia ata admission kwaajili ya mdogo/mwanao.


5. Fukwe
Kuna fukwe nzuri na kubwa ambapo pia utaona shughuli mbalimbali za uvuvi. Fukwe zao ni bure na hazina viingilio.



Kuhusu malazi, Bagamoyo ina lodge za bei ya kawaida lakini pale mji mkongwe kuna hotels za kitalii na cottage za kishua ambazo kulala inazidi ata laki 1 kwenda juu.


Ukitaka kuona mji vizuri, tumia usafiri wa baiskeli au pikipiki kwasababu utaona mengi zaidi na utafaidi.



Sehemu zingine unaweza visit:
1. Snake Park (Kuna aina mbalimbali ya nyoka, wanyama (zoo), michezo mbalimbali ya watoto na wakubwa. Ipo Kaole road, karibia Kilometa 5 kutokea mjini Bagamoyo.
2. Empire Sport Bar Kanywe bia.
3. Kaole Ruins kwa picha na more history.
4. Poa Poa Restaurant kale Pizza.

Picha nyingine:
 

Attachments

  • PXL_20240324_104914937.jpg
    4.7 MB · Views: 90
Yeah mfano msimu wa mvua kunavutia sana.
Asante kwa thread nzuri. Hivi hakuna orginized tour eg kunakuwa na na gari la wazi linalozunguka maeneo yote yenye vivutio? Kama hakuna wanajaribu kufanya hivyo kama nchi za Ulaya zilivyo. Unakuwa na bus la wazi, lenye mic na headphones linakuwa linafanya vituo maalumu na root ya kuzunguka sehemu zote za vivutio. Mtalii akifika kituo sehemu yenye kivutio anaweza ku-drop akabaki pale kwa muda na kwa sababu bus linazunguka muda wote, likija anapanda tena kuelekea sehemu nyingine.
 
Namaanisha nature ya udongo wa kule na matope ya huko hasa kipindi cha mvua, mtu ukija na gari lako binafsi ujipange kwenye barabara za ndani huko ambapo hamna lami
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚Hivyo vivutio vyote vipo hapo town tu Wala huendi interior... it's a nice place kuosha macho,unawezA jihisi kidogo uko Stone town
 
Ahsante ndugu mwandishi. Naitwa James ni tour guide hapa Zanzibar so far nina plan ya kutoka hapa kwenda Bagamoyo kufanya utalii wa ndani na kwa sasa umenipa mwanga.
Ahsante sana..
Tarehe 9.april.24 nitaanza safari, anaehitaji ku_join anakaribisha sana. Anicheki kwa e_mail yangu
Karibuni pia Zanzibar
 
Panavutia kivip Mana nina plan ya kutoka hapa na kwenda huko kipindi hiki cha mvua,
Niliwahi kufika Majura ya mvua na jua..Hakuna usumbufu kabisa.Niliwacha usafiri pale Magofu karibu na BADECO..Mwenyeji mmoja akanioeleka kukodi baiskel....Nilitalii Sana..
Next days,nilikenda Tena na kukunua shamba...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…