Bagamoyo: Mitishamba ya kuongeza nguvu za kiume yadaiwa kusababisha vifo vya vijana Wanne

Bagamoyo: Mitishamba ya kuongeza nguvu za kiume yadaiwa kusababisha vifo vya vijana Wanne

Matatizo ya ukosefu wa nguvu za kiume uchangiwa na mambo makuu manne.
1.Ukikosa pesa..
2.Msongo wa mawazo unaosababishwa na namba 1
3.Matatizo ya kisaikolojia.
4.Kutokula chakula Bora.
Sasa hapo utachemsha hadi majani ya mmavi mavi lakini wapi.
Vijana wasiku hizi hawana pulling kwa sababu chips mayai mimi nipo na miaka 48 lakini nipo na uwezo wakupiga bao moja kwa dakika 45 kwa siku nakwenda bao 2 mpaka asubuhi 3
 
Ni kweli kabisa.
Umalaya ndio chanzo cha haya yote. Imagine mwanamke ameanza uhsiano na mwanaume mmoja na akadumu nae, ni lini atajua kama kun kibamia na big size.
Kiukweli maumbile ya me na ke hayawezi kufanana kwa size na hiyo ni tangu enzi za mababu. Ila sasa hivi inaonekana tatizo sababu ya umalaya.
Mwanamke ukidate na wanaume 5+ lazima u come up na hoja za kibamia coz wote hawawezi fanana size.

Wabadilike na wawe wavumilivu kama ambavyo walikua mama zao na bibi zao,wenye maumbile madogo walikuwepo tangu zamani hizo ila uwezo wa kinamama wa kipindi hicho wa kuhifadhi mambo ya ndani ulikua mkubwa sana
 
Vijana wanne wamepoteza maisha baada ya kunywa dawa ya kienyeji ya mitishamba inayodaiwa ya kuongeza nguvu za kiume.

Mkasa huo umetokea Huko Bagamoyo Maeneo ya Kiromo, ambapo vijana hao ambao kwa umri wao ni kama miaka 25-30.

Kwa mujibu wa taarifa ya mmoja wa marehemu alijulikana kwa jina la Elisha kabla ya umauti haijamkuta anasema mwenzao ambaye pia ni marehemu hivi sasa ndiye ambaye aliwauzia dawa hiyo ya miti shamba ambapo kwa nyakati tofauti marehemu hao walikunywa na kusababisha vifo vyao.

Anasema yeye alinunua dawa hiyo kwa tsh 2,000 na kupewa dozi hiyo na kuanza kuinywa siku ya alhamis ya wiki iliyopita, siku ya jumamosi asubuhi alianza kujisikia vibaya huku akiwa anaharisha sana na kutapika, hali iliendelea kuwa mbaya zaidi hivyo kupelekwa hospital ya wilaya ya Bagamoyo kwa matibabu zaidi hata hivyo hali alizidi kuwa mbaya zaidi kwani alikuwa anatapika mabonge ya Damu ndipo mauti ikamkuta majira ya saa 8:40, Mwili wa Elisha umeagwa leo kwenda kuzikwa huko Ukerewe.

Wakati Elisha anapambana na mauti mwenzake anayejulikana kwa jina la Mjahusi ambaye ndiyo alikuwa mtayarishaji wa dawa hiyo alikuwa naye anapatiwa matibabu hospital hapo yeye alipata mauti usiku wa kumkia siku ya jumapili.

Taarifa zinasema kuwa wengine wawili walifia kigamboni na Bunju walikukuwa wanaishi.

Aidha kijana mmoja anajulikana kwa jina la Lowasa yeye hali yake bado si nzuri na amelazwa hospital maeneo ya Tegeta.

Kwa mujibu wa mmoja wa aliyenusurika ajulikanaye kwa jina Muha anasimulia akisema kwamba walinunua yeye na wenzake dawa hiyo kwaajili ya kuongeza nguvu za kiume na walikuwa wanatumia zaidi ya mara moja hawakupata na tatizo lolote tofauti na hiii waliotumia ikawaletea madhara makubwa.

Muha anasema muuzaji na mtengenezaji wa dawa hiyo awali alikuwa anaigiza dawa kutoka Bukoba lakini baada ya muuzaji kugundua mti uliokuwa unatengeneza dawa hiyo unapatikana pia Maeneo ya Bagamoyo aliamua kutengeza dawa hiyo kwa mizizi ya mti huo hali sababisha tafrani na watu kupoteza maisha.

Muha anasema kilichomsaidia yeye ni kwamba baada ya kuinywa alipoanza kujisikia vibaya alikunywa maziwa na maji mengi ndiyo ilikuwa salama yake.

Picha ya kwanza Mwili wa Elisha ukiagwa
Picha ya pili Muha akiwa kwenye msiba wa rafiki yake Elisha.
Vijana hawapaswi kukosa nguvu za kiume hadi kufikia kutegemea mitishamba.
 
Huwezi kujua huyu ni mrefu bila mfupi kuwepo, na huwezi kujua huyu ni mnene bila mwembamba kuwepo, wanawake wapunguze umalaya!!
 
Back
Top Bottom