Bagamoyo sugar project ilkua biashara ya kitapeli

Wewe eneo lako unasema mwenyewe au inakusemea serikali na je serikali haimiliki ardhi? Sasa kwa nini SMZ isiseme kama eneo fulani wanalimiliki wao na hatimiki wanayo!
Mkuu, kwani na wewe ni shabiki wa Yanga?

Mamlaka sio MTU binafsi! SMZ haina hiyo jurisdiction! Kwanini wasingepitia proper channels kama serikali?

Bakhresa, yeye ndo atangaze kisha kama kuna mgogoro, JMT inaamua kupitia vyombo vyake! Sasa kweli SMZ iwe kama Bakhresa?

Mwisho, nimekuuliza, sheria inasemaje kuhusu kuiacha ardhi kwa zaidi ya miaka 10 bila kuiendeleza?
 
Serikali ni kama mtu ndio maana inaweza kushtakiwa ama kushtaki kama mtu binafsi.
Una uhakika hiyo ardhi haijaendelezwa kwa sababu madaraka ya kusimamia ardhi yamekasimiwa kwa Kamishna wa ardhi ambaye kama ataona mmiliki aliyemilikishwa ardhi ameshindwa kutekeleza masharti ya umiliki basi atapendekeza kwa Rais ambaye ndiyo mdhamini wa ardhi yote nchini kwa niaba ya Watanzania aifute hati ya umiliki ya muhusika lakini hadi leo Shamba hilo bado linamilikiwa na SMZ kupitia wizara yao ya kilimo hii maana yake hawavunja masharti yoyote ya umiliki.
 
Shamba hilo bado linamilikiwa na SMZ kupitia wizara yao ya kilimo hii maana yake hawavunja masharti yoyote ya umiliki.
Unajiaminisha utafikiri unaishi mbinguni, hujui yanayoendelea Tanganyika sio?

Eti haijavunja masharti! Unaifahami ripoti ya CAG? Hatua hazijachukuliwa, je, inamaanisha hakuna uwalakini?
 
Unajiaminisha utafikiri unaishi mbinguni, hujui yanayoendelea Tanganyika sio?

Eti haijavunja masharti! Unaifahami ripoti ya CAG? Hatua hazijachukuliwa, je, inamaanisha hakuna uwalakini?
Unataka waje kukugongea kwako kukwambia kwamba wameanza kuchukua hatua.
 
Bagamoyo Sugar Project ilikuwa biashara ya kitapeli?
Sio kweli. Nia ilikuwa nzuri- kukuza ushirikiano kati ya Tz na Sweden katika kuzalisha sukari na nishati. Kilichokwamisha uwekezaji ni pamoja na migogoro ya ardhi ikiwemo maslahi ya wanavijiji, kuchukuwa muda mrefu kuamua matatizo n.k. Serikali ya Sweden ilijitoa kukabaki kampuni binafsi za Sweden zilizoshitaki Tz- kampuni za EcoDevelopment na EcoEnergy.
Muwekezaji kukopa toka benki au mahala pengine ni jambo la kawaida, SI KUWA TAPELI.
Tusubiri mahakama itaamueje.
 
Kama ndivyo upangaji wa hoja umevurunda
Umecharaza hovyo!!
 
Kama Bakhresa alipewa na Magufuli ili alime sukari na anafanya hivyo..
Case closed...
Kisheria Rais wa nchi anaweza batilisha matumizi ya ardhi popote
 
Mkuu umeandika fact ila na mm nafikir huyu wa sasa ndio anataka kuwakabidhi nduguze ...

Haiwezekan, maana ukisoma machapisho ya project yanaonyesha ilo eneo lilirejeshwa kwa wawenye miaka ya 1990's iweje leo wajitokeze wadai ni mali yao ?
 
Mkuu umeandika fact ila na mm nafikir huyu wa sasa ndio anataka kuwakabidhi nduguze ...

Haiwezekan, maana ukisoma machapisho ya project yanaonyesha ilo eneo lilirejeshwa kwa wawenye miaka ya 1990's iweje leo wajitokeze wadai ni mali yao ?
Ujumbe umfikie huyo mzanzibar anayetoa pesa bara kupeleka visiwan
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…