Bagamoyo

Bagamoyo

CHE GUEVARA-II

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2010
Posts
571
Reaction score
156
Wadau, habari zenu?
Naomba mnijulishe.
Bagamoyo (Kiwangwa) ni mazao gani ya biashara yanastawi ili kuuza kwa wafanyabiashara wakubwa kama kina Bakhresa au hata kimataifa au hata mazao yanayoweza kumwezesha mtu kuvuta mkopo wa maana bank?
Mfano: maembe, mananasi, michungwa n.k
Au hata miti ya mbao (tectona grandis = teak trees = mitiki) au nasikia kuna miti fulani ambayo products zake zinatumika kutengenezea vyombo vya majini - sijui inaitwaje! Naomba mwongozo wenu.

Kuna mdau anataka aendeleze ekari zake 50 huko Kiwangwa.
 
Asante kwa ushauri.
Miti ya mbao (mitiki) haiwezi kustawi Kiwangwa?

angalia hali ya hewa ya hapo Kiwangwa mkuu na uhitaji wa hali ya hewa ya hicho unachotaka kupanda.
Kama 1+1 = 1 then panda. Ila kama 1+1=2 potezea.
Najua ni ngumu kumeza ila meza tu hivyo hivyo
 
Asante kwa ushauri.
Miti ya mbao (mitiki) haiwezi kustawi Kiwangwa?

Mananasi Kiwangwa ndio kwao,hadi wayahudi wanayafuata shambani moja kwa moja, pili embe zaweza kufanya vizuri pia kwa sababu chache za kisasa na za kienyeji ziko vizuri, kando ya Kiwangwa kama unapandisha Msata waweza lima mahindi na jamii nyingine za nafaka.

Nimepita juzi,kijiji kimoja kabla ya Fukayosi, kuna jamaa ameotesha eucalyptus saligna/grandis, miti hii iko vizuri na inakuwa kwa speed kubwa, kwa sasa ina soko la kufa mtu ktk umri wo wote kuanzia miaka mitano na kuendelea. Tatizo lake inaliwa sana na rodents pamoja na mbuzi. Na ukishapanda mti huo, shamba hilo hutaweza kulima tena labda ufugaji, miti hii visiki vyake having`oki na havifi kirahisi, ukikata kinachipua vizuri.

Mitiki unaweza kuotesha kama ardhi yako ni wet ila kama ni kavu kama ya Chalinze, miti itakuwa kwa taabu sana na haitakuwa minene, ukame ukipita kidogo tu, miti inakufa sana. Kama utapanda vizuri na usimamizi mzuri, basi tia timu.
 
Mheshimiwa Malila asante kwa maelezo mazuri. Hivi nanasi huhitaji mvua kwa wingi au la? Ukanda wa pwani una mvua za kubahatisha.
 
Ili kupata mavuno mazuri,mvua ni lazima. Ukanda wa Kiwangwa kuna mvua nzuri na udongo mzuri kwa kilimo, ndio maana mitaa ile yote ya Msata,Mandela,Kiwangwa,Madesa mpaka Kabuku mahindi yanamea na kuzaa vizuri. Madesa niliona hadi maharage, nikashangaa sana.
 
Back
Top Bottom