Mananasi Kiwangwa ndio kwao,hadi wayahudi wanayafuata shambani moja kwa moja, pili embe zaweza kufanya vizuri pia kwa sababu chache za kisasa na za kienyeji ziko vizuri, kando ya Kiwangwa kama unapandisha Msata waweza lima mahindi na jamii nyingine za nafaka.
Nimepita juzi,kijiji kimoja kabla ya Fukayosi, kuna jamaa ameotesha eucalyptus saligna/grandis, miti hii iko vizuri na inakuwa kwa speed kubwa, kwa sasa ina soko la kufa mtu ktk umri wo wote kuanzia miaka mitano na kuendelea. Tatizo lake inaliwa sana na rodents pamoja na mbuzi. Na ukishapanda mti huo, shamba hilo hutaweza kulima tena labda ufugaji, miti hii visiki vyake having`oki na havifi kirahisi, ukikata kinachipua vizuri.
Mitiki unaweza kuotesha kama ardhi yako ni wet ila kama ni kavu kama ya Chalinze, miti itakuwa kwa taabu sana na haitakuwa minene, ukame ukipita kidogo tu, miti inakufa sana. Kama utapanda vizuri na usimamizi mzuri, basi tia timu.