Bagia zinapikwaje?

Joined
May 8, 2012
Posts
29
Reaction score
4
Naomba msaada Wana JF wa kufahamu jinsi zinavyotengenezwa BAGIA za Dengu na Kunde.
 
MAHITAJI
KUNDE nusu kg
pilipili kiasi
karoti 3 kubwa
hoho
kitunguu
hamira kidogo kama robo kijiko
unga wa ngano vijiko vitano
hiliki
kitunguu swaumu

1.Loweka kunde like lets say usiku thn kupika upike kesho yake
2.kata vitunguu,hoho,karoti kwenye umbo la cubes za mraba
3.twanga au blend kunde (unaweza kutoa maganda au ukasaga pamoja)
4.changanya viungo vyoooote kisha weka hamira na ngano mwishoni
5.tengeneza madonge madogo madogo kulingana na kiasi unachopenda
6.bandika mafuta yachemke kisha anza kukaanga
7.acha mpk ziwe kahawia

ANDAA!na juice poa,chai poa,maziwa mwake basi mradi raha
cc Kaunga
 
Last edited by a moderator:

Ujue umenirudishia spirit ya kupikapika ambayo ilikuwa imekufa; anyway kwa vile wanyamwezi wanapenda mizigo ngoja niendelee kuchopoa tu so makalio yakiambatana na tumbo yazidi kuongezeka.
cc: The Boss, KIKUNGU, Mkirua
 
Ujue umenirudishia spirit ya kupikapika ambayo ilikuwa imekufa; anyway kwa vile wanyamwezi wanapenda mizigo ngoja niendelee kuchopoa tu so makalio yakiambatana na tumbo yazidi kuongezeka.
cc: The Boss, KIKUNGU, Mkirua
hahahahahhahaha kuhusu Mkirua huyu itabid nikufundishe ule mtori wa ndizi na maghimbi
hao kaka zako kwa kweli unipe tu marecipe ya kuwatega siku moja moja ,lol!
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…