Bagonza: Chadema ina mashabiki wengi kuliko wanachama. CCM ina wanachama wengi kuliko mashabiki.

Bagonza: Chadema ina mashabiki wengi kuliko wanachama. CCM ina wanachama wengi kuliko mashabiki.

Baraka Mina

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2020
Posts
586
Reaction score
590
Askofu Dkt. Bagonza

HONGERA CHADEMA, lakini.……

Mkutano wenu umeonyesha haya:

- Chadema ina mashabiki wengi kuliko wanachama. CCM ina wanachama wengi kuliko mashabiki.

- Kazi ya Chadema ni kubadili mashabiki kuwa wanachama, na ya CCM ni ya kuongeza mashabiki bila kupoteza wanachama. Msichukiane, msipendane, msimalizane bali mjifunze kuishi na hali msiyoweza kuibadilisha.

- Wanachama wanapenda kuchagua viongozi wao. Hujuma kutoka kwa wapinzani wenu zina nguvu sawa na hujuma za kutengeneza wenyewe. Jilindeni na chachu ya ubaguzi, ukanda, U-wenyewe na ubabe. Haya ni mabaya mkiyaona kwa watani wenu; hayawezi kuwa mazuri ndani yenu.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom