KWELI Bahari ya Galilaya yageuka Nyekundu kama damu

KWELI Bahari ya Galilaya yageuka Nyekundu kama damu

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Nimekutana Na Chapisho Kwenye Mtandao Wa Instagram Likieleza Kuwa Bahari Ya Galilaya Imegeuka Nyekundu Kama Damu
Chapisho Hilo Limechapishwa Kwenye Ukurasa Wa Global Tv Online's
Nimeona Nilete hapa Kwa Ajili ya Verification


1754894491091.png
 
Tunachokijua
Madai

Kumekuwa na taarifa kuwa bahari ya Galilaya nchini Israel imegeuka kuwa nyekundu kama damu. Tazama hapa na hapa

Uhalisia wa taarifa hiyo

JamiiCheck imefuatilia na kujiridhisha kuwa taarifa hiyo ni ya kweli.

Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii watumiaji walichapisha taarifa hiyo ya bahari ya Galilaya kuwa nyekundu na kuhusianisha tukio hilo na lile lilitokea kwenye biblia katika kitabu cha kutoka ambapo ilikuwa ni moja ya mapigo ya Mungu kwa Wamisri. Watu wengi walikuwa na imani kuwa sasa ni mwisho wa dunia utakuwa umekaribia.

Wanasayansi wao wamekuwa na mtazamo tofauti kuhusiana na jambo hilo ambapo wizara ya mazingira nchini Israel ilieleza kuwa rangi hiyo nyekundu ilisababishwa na mwani ambao kwa asili ni wa kijani, lakini hubadilika na kuwa mwekundu unapoathiriwa na mwanga mkali wa jua, joto la juu na maji yenye virutubisho vingi.

Maafisa wa Israel walibainisha kuwa mwani huo hauna sumu wala madhara ambapo pia vipimo vimefanyika na kujiridhisha kuwa maji hayo ni salama kwa uogeleaji.
Back
Top Bottom