TANZIA Baharia Mtanzania apoteza maisha wakati meli inavuka mfereji wa Hormuz

TANZIA Baharia Mtanzania apoteza maisha wakati meli inavuka mfereji wa Hormuz

MakinikiA

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2017
Posts
5,840
Reaction score
8,202

Waajemi msiwasogelee jamani..​

Meli
Chanzo cha picha,Getty Images

Baharia wa Kitanzania amepoteza maisha wakati akihudumu katika meli ya kuvuta iitwayo VOLANS, Shirika la uwakala wa Meli Tanzania, TASAC limeeleza.

Kifo cha baharia huyo kwa jina Mchama Maregesi Mongu, kilitokea tarehe 3 mwezi Mei mwaka 2026.
Meli hiyo iliyobeba bandera ya Umoja wa Falme za Kiarabu, ilikuwa safarini kutokea UAE kuelekea nchini Oman.
Chombo hicho kilishambuliwa na bomu wakati kikivuka kwenye mlango bahari wa Hormuz uliopo kati ya nchi za Iran na Oman.

Katika taarifa yake, TASAC imesema kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki zinafuatilia kwa karibu taarifa za tukio hilo ili waweze kuurudisha mwili wa marehemu nchini Tanzania, mara tu utakapopatikana.

''TASAC inaungana na IMO kusisitiza umuhimu wa kulinda maisha ya mabaharia wanapokuwa baharini, hususani katika maeneo yanayohusisha haki ya kupita kwa amani kama inavyolindwa na Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa sheria ya bahari'' Ilisema taarifa hiyo.

Unaweza kusoma;
Mlango-Bahari wa Hormuz: Nini kitatokea Iran ikifunga njia ya usafirishaji mafuta?

Baharia Hormuz.jpg
 
Usiguse huu waya una umeme unasema hapana ngoja niguse nihakikishe ..
Mungu akumweke mahali pema peponi.
 
Hakuna hatua zozote zinazochukuliwa dhidi ya iran zaidi ya kuurudisha mwili wa marehemu?
 
Ujinga wa Israel na Marekani unatuathiri tusiohusika,
Trump **** lako la nyuma pamoja na mwenzio.
 
Inasikitisha sana ,matajiri wa meli ebu jaribuni kuangalia maisha ya wafanyakazi wenu kwanza ,wewe ushaona kwamba hapo HORMUZ ni balaa ,nje ntiti ndani ntinti yanini upitishe meli wakati usalama ni mdogo?
 
Back
Top Bottom