- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Je, ni kweli kuna Samaki mtu? Maana huku mtaani kuna watu huwa wanatuhadithia namna walikutana na Samaki watu au kuhadithiwa na wengine stori kama waliona mwanamke Mrembo mweupe kama Mwarabu ila amekaa juu ya jiwe au ufukweni au anaogelea kwenye bahara au ziwa.
Mwanamke huyo wanaeleza anakuwa na nywele ndefu na chini umbile la samaki wa kawaida ila kuanzia kiunoni ndio binadamu, na wasimuliaji husimulia kuwa ukitaka kumkamata unaona analia na anaomba usimkamate wengine wakidai wana watoto wadogo wananyonyesha, au wana familia hivyo kuomba waachwe huru waondoke.
Stori ni nyingi sana huku wakidai samaki watu hao hukamatwa na kuliwa kama samaki wengine huku viwiliwili vyao vikizikwa au kutupwa tena majini.
Je, ukweli ni upi JamiiCheck msaada katika hili.
Mwanamke huyo wanaeleza anakuwa na nywele ndefu na chini umbile la samaki wa kawaida ila kuanzia kiunoni ndio binadamu, na wasimuliaji husimulia kuwa ukitaka kumkamata unaona analia na anaomba usimkamate wengine wakidai wana watoto wadogo wananyonyesha, au wana familia hivyo kuomba waachwe huru waondoke.
Stori ni nyingi sana huku wakidai samaki watu hao hukamatwa na kuliwa kama samaki wengine huku viwiliwili vyao vikizikwa au kutupwa tena majini.
Je, ukweli ni upi JamiiCheck msaada katika hili.
- Tunachokijua
- Samaki mtu au kwa jina jingine Nguva ni wanyama wakubwa wanaoishi baharini. Hata hivyo ni mamalia wanaozaa watoto walio hai na kuwalisha kwa maziwa. Nguva huwa na mikono ya mbele na mkia wenye umbo la pembetatu. Wanaishi kwenye pwani za Bahari ya Hindi, Bahari ya Karibi, Afrika ya Magharibi na mto wa Amazonas. Wanaweza kufikia urefu wa mita 2.5 hadi 4 na uzito wa kg 1,500. Jina la Kisayansi ni Sirenia.
Nguva ni kiumbe ambaye amejizolea umaarufu mkubwa sana duniani, lakini umaarufu wake huo huishia kwenye jina tuu na si muonekano wake, kiuhalisia kiumbe huyu akionekana ni vigumu sana binadamu kumtambua kwamba ndiye nguva mwenyewe ambaye humzungumza nyakati tofauti, na yote hiyo ni kutokana na uvumi ambao umeenezwa ya kwamba eti nguva ni nusu mtu pia nusu samaki, tena samaki ambaye ni mwanamke, pamoja na uvumi huo lakini hata siku moja haikuwahi oneshwa viumbe hao madume wake hufanania vipi, pia haijawahi thibitishwa kwamba dume la nguva huyo avumaye naye huwa na muonekano huo huo wa samaki mwanamke.
Kumekuwa na masimulizi mbalimbali juu ya kiumbe kiitwacho Nguva/Samaki Mtu huku wasimuliaji wakidai nguva ni kiumbe kinachoishi baharini chenye umbile lililogawanyika mara mbili, Kiwiliwili ni Mtu na Kuanzia kiunoni ni Samaki huku kukiwa na picha mbalimbali kuonesha uwepo wa viumbe hivyo ambavyo hudaiwa kuzungumza kama wanadamu.
Je, Ukweli ni upi?
JamiiCheck imepitia Tafiti mbalimbali na kubaini kuwa Nguva ni wanyama wakubwa wanyonyeshao na Siyo Samaki na Mtu kama ambavyo watu wanavyodai kwamba wana kiwili wili cha mwanadamu na mkia wa samaki (samaki mtu), Baharini, Ziwani na mitoni hakuna kiumbe kama hicho na wl hakijawahi kuwapo, wala huwezi kukikuta katika bahari yoyote duniani.
Nguva si samaki kama ivumishwavyo, Kiumbe huyo ni mnyama aishiye majini kama alivyo kiboko tuu, kwa jina jingine huitwa Ng'ombe wa majini na majike yake huvuma kwa jina la malkia wa majini.
Nguva ni miongoni mwa wanyama wanaoishi miaka mingi sana na huzeeka akiwa na miaka 50 na huweza huweza kufika hata 70 na zaidi ikiwa atapata malisho mazuri. Chakula chake kikuu ni majani, hupevuka wafikishapo miaka 9 mpaka 16 na mimba hubeba kwa miezi 13 mpaka 15, Nguva huzaa mtoto mmoja tuu, muda mfupi baada ya kuzaliwa mtoto hupelekwa juu ili apate nafasi ya kupata pumzi vyema na hunyonya kwa miezi 18 baada ya hapo hujifunza kutafuna majani na siku atakapopevuka tuu huacha kukaa na mama yake. Na nguva wana matiti mawili kifuani na wana haiba ya aibu.
Viumbe hawa walianza kuzungumziwa tangu zamani kwenye hadithi za kale za mataifa mbalimbali huko Asia na Ulaya lakini katika maisha halisi hawapo, wengine wanasema samaki hao wanaweza wakaongea kama mwanadamu, lakini hilo jambo si kweli kwani hivyo viumbe havipo.
Kwa Mujibu wa Tovuti ya National Ocean Service ya Nchini Marekani inaeleza kuwa Samaki Mtu ni viumbe wa kufikirika waliokuwa wanatajwa kwenye hadithi za tamaduni za baharini tangu enzi za zamani. Aidha, wanaeleza Hakuna ushahidi wa kuwepo kwa viumbe wenye sifa za nusu binadamu na nusu Samaki uliopatikana.
Aidha, kwa mujibu wa Abyss Scuba Diving Wanaeleza kuwa Nguva(Nusu mtu nusu samaki) hubakia kuwa somo la kuvutia la hadithi, linalosimulia hadithi za Kufikirika za kale, maisha ya baharini ambayo hayajawahi kuwepo ambapo hadithi hizi zimewahi kuandikwa na Mshairi wa kale wa Kigiriki Homer aliandika katika "The Odyssey"