Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 23,526
- 34,057
BAHASHA ILIYOBEBA KITABU KUTOKA KWA ALLY DAR ES SALAAM KWENDA KWA ALI NAIROBI
Asalaam Aleikum Warahmatullah Wabarakatuh Sheikh Salim,
Ahsante sana kwa kuniletea kumbukumbu ya Balozi Chirau Ali Mwakwere aliyoihifadhi ya Ally Sykes.
Tulikuwa sote msibani na wewe ndiye yliyonifahamisha kuwa Balozi Ali Mwakwere ana hamu ya kukutana na mimi.
Nilikutananae Pande wakati wa maziko ya Juma Mwapachu.
Balozi Ali Mwakwere anasema kuwa alionana kwa mara ya kwanza na Ally Sykes Muthaiga Country Club, Nairobi na ndiyo ikawa sababu ya yeye kuletewa kitabu cha Abdul Sykes na Ally Sykes katika bahasha hiyo aliyoihifadhi hadi leo.
(Ningependa kukufahamisha kuwa mimi niliingia Muthaiga Country Club mwaka 1989 na aliyeniingiza mle ndani ni Ally Sykes.
Muthaiga Country Club si mahali pa kila mtu kutia mguu wake).
Kitabu hiki Ali Mwakwere alitueleza kuwa kilimuathiri sana na ndani ya kitabu kile ndipo alipomsoma Kleist Sykes baba yao Abdul, Ally na Abbas.
Hapa ndipo alipoikuta historia ya kweli ya kupigania uhuru wa Tanganyika.
Balozi Ali Mwakwere akatueleza kuwa yeye amehifadhi hadi leo bahasha ambayo Ally Sykes alimletea kitabu cha Abdul Sykes.
Tarehe katika bahasha ile inaonyesha ni tarehe 12 March 2008.
Miaka 17 iliyopita.
Nashukuru kuwa Balozi Ali Mwakwere amekuletea wewe rafiki yake toka mlipokuwa shule pamoja Shimo la Tewa bahasha hiyo aliyoletewa kitabu cha Abdul Sykes na wewe umeniletea mimi.
Kwa kweli umenifurahisha sana. Nami namuomba Allah akufurahishe kama ulivyonifurahisha mimi.
Napenda kuhitimisha kwa kukumbusha kuwa pale mazikoni ulinikumbusha siku tulipokutana mpaka wa Horohoro mwaka jana.
Mimi nilikuwa natoka Mombasa kwenye harusi ya binti wa rafiki yangu Abdulaziz Ali Khamis.
Abdulaziz Ali Khamis ukoo wao ni maarufu Guraya, Mombasa na umaarufu wao unatokana na Allah kuwajaalia elimu ya juu ndugu wote wa kike na wa kiume.
Naamini kwa kuwa wewe ulikulia Mombasa utawafahamu.
Abdulaziz kaniambia kuwa Balozi Mwakwere wanafahamiana vizuri kwani wakicheza golf pamoja Vet Lab Golf Club, Nairobi.
Hakika dunia hii ni ndogo sana.