Bahati Bukuku ni mama, Rose Mhando Ni kabinti kwenye uandishi

Bahati Bukuku ni mama, Rose Mhando Ni kabinti kwenye uandishi

Huyu jamaa kazingua Sana lakini tuheshimu maoni yake lakini ukweli utabaki kua ukweli Rose Muhando ndiye mwimbaji na mtunzi Bora wa Gospel Kwa wamama tangu Tanzania ianze..

Kuna Ngoma za Rose ambazo zikipigwa hata sasa hivi utatamani kuokoka...

Hebu leta Ngoma za bahati bukuku zenye utunzi maridadi kuliko hizi za Rose hapa Chini...

Nipe uvumilivu
Wanyamazishe
Nakaza mwendo
Mteule uwe macho
Yesu Nakupenda
Si Salama
Mapambio
Raha
Hatumo
Nibariki

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni Rose atabaki kua legend Hadi kiama. Huwezi mlinganisha Zinduna na Mzee tupatupa
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mbona mzee tupa tupa!! Woiiiiih
 
Kila mmoja ni mzuri kwa angle yake.

Mhando
Mteule uwe macho ilikuwa mbele ya muda kipindi hicho
Nipe uvumilivu
Kina mama wa leo
Yesu nakupenda
Ndivyo ulivyo
Holini mwa ng'ombe


Bukuku
Ni nyakati za mwisho
Mapito
Ikulu ya Mbinguni
Siri
Nakutegemea
Tutakaposimamishwa kizimbani pale

Yaani wote wakali aisee,kila mtu na flavor yake
Rose, ikipigwa "nibebe" mbona upako unashuka mahali hapo muda huo huo.

Rose ni mkali bhana
 
Nimepitia maoni yote nasikitika hakuna aliyeweza kumpa Rose Muhando heshima yake stahiki.

Hakuna mwanamuziki wa kike aliyewahi kutokea nchi hii kama Rose Muhando, kuanzia uandishi hadi uimbaji. Wengi mnachanganya mapito aliyopitia katika maisha yake binafsi kumnyima heshima yake, sio sawa.

Ama kweli nabii hakubaliki nyumbani! Nchi nyingine wanatamani Rose angekuwa mzaliwa huko kwao. Nendeni Rwanda muone, Kenya je? Sijaongelea Kongo.
Upanga uitwe upanga, Rose ni gwiji.
Haipingwiiiiii!!!
 
Back
Top Bottom