Bahati nasibu ya Taifa yashirikiana na Selcom Tanzania

Bahati nasibu ya Taifa yashirikiana na Selcom Tanzania

News TZ

Senior Member
Joined
Jun 17, 2015
Posts
169
Reaction score
88
WhatsApp Image 2025-04-07 at 10.56.28 AM.jpeg

Bahati Nasibu ya Taifa ya Tanzania, leo imetangaza rasmiushirikiano na mtoa huduma kinara wa malipo kwa njia ya simu nchini Selcom Tanzania, ilikuhakikisha Watanzania wanashiriki katika michezo ya bahati nasibu kwa urahisi mara tuBahati Nasibu ya Taifa itakapozinduliwa rasmi. Ushirikiano huu utarahisisha upatikanaji,ununuzi na ulipaji wa tiketi kwa urahisi na usalama kote nchini.

Ushirikiano huu na Selcom Tanzania ni hatua muhimu katika kuhakikisha kuwa Bahati Nasibuya Taifa inawafikia Watanzania wote nchini. Kwa kutumia miundombinu madhubuti ya malipoya Selcom, Wachezaji wataweza kushiriki katika michezo ya bahati nasibu kupitia USSD codes, Kuhamisha kutoka benki, mawakala wa selcom huduma ambao wapo zaidi ya 30000 nchinzima,na vituo vya selcom 10 vilivyopo maeneo mbalimbali hapa nchini. Pia washiriki wabahati nasibu ya taifa wataweza kununua tiketi na kupokea malipo ya ushindi kupitia majukwaaya fedha kwa njia ya simu, USSD, hamisho kutoka benki, vituo vya malipo ya Selcom, namiamala ya kidijitali. Aidha, upatikanaji wa Selcom katika taasisi mbalimbali za kifedhautahakikisha kuwa hata wale wanaoishi maeneo yasiyofikika kiurahisi wanaweza kushirikikikamilifu katika michezo ya bahati nasibu ya taifa.

Mkurugenzi wa ITHUBA Tanzania, Bw. Kelvin Koka, ameelezea umuhimu wa ushirikiano huuna Selcom Tanzania. Amesema, "Hii ni ni hatua kubwa katika sekta ya michezo ya kubahatishanchini, kwa kushirikiana na Selcom, tutahakikisha kuwa Bahati nasibu ya Taifa itakapozinduliwa kila Mtanzania bila kujali mahali alipo nchini, ataweza kushiriki kikamilifukatika michezo mbali mbali ya kusisimua ya bahati nasibu.

Bahati nasibu ya Taifa si michezo ya kubahatisha tu bali pia ni chombo cha maendeleo ya taifa.Sehemu ya mapato yatokanayo na mauzo ya tiketi za bahati nasibu yatatengwa kwaajili yamiradi muhimu kama vile kuendeleza michezo ya vijana chipukizi, na sekta nyingine zinazoigusa jamii. Ushirikiano huu na Selcom utakuwa na mchango mkubwa katika kuongeza ushirikiwa umma, hatimaye kuongeza mchango wa pato la Taifa kupitia miradi hii.

Usalama ni nguzo kuu ya ushirikiano huu, ambapo kupitia teknolojia bora ya Selcom washirikiwataweza kununua tiketi, kupokea malipo kidigitali kwa usalama ambao utazuia udanganyifuwa aina yoyote.

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa ushirikiano huu, Shumbana Walwa, Mkuu wa idaraya Masoko wa Selcom Tanzania amesema, "Ushirikiano wetu na Bahati nasibu ya Taifa yaTanzania unalenga kurahisisha ushiriki katika michezo ya kubahatisha kwa kila Mtanzania.Kupitia miundombinu yetu imara ya malipo, tutahakikisha kuwa mara tu Bahati nasibu ya Taifa itakapo zinduliwa, wachezaji wataweza kushiriki kwa urahisi kupitia njia ambazo tayari wanaziamini na kuzitegemea. Tumejidhatiti kutoa huduma ya malipo salama, bora, na yakuaminika ili kuongeza urahisi wa upatikanaji wa michezo ya bahati nasibu na ushiriki."

Kwanzia sasa, Bahati nasibu ya Taifa ya Tanzania na Selcom wataendelea kushirikianakuhakikisha kuwa Watanzania wanapata uzoefu wa kusisimua wa michezo ya bahati nasibuitakayopatikana katika jukwaa la Bahati nasibu ya Taifa, kwa usalama na uwazi wenye manufaakwa watu binafsi na taifa kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom