Keagan Paul
JF-Expert Member
- Jul 19, 2018
- 510
- 3,178
Niliwahi kusoma kisa kimoja cha kijana aliyekamatwa kwa kosa la uzururaji. Alipofikishwa kituo cha polisi alitakiwa atoe cho chote ili aachiwe, yule kijana akagoma.
Kesho yake alipofikishwa mahakamani, yule kijana alisomewa shitaka la kuendesha baiskeli isiyokuwa na taa! Akakiri kosa na kupigwa faini shilingi ishirini. Akalipa faini na badae akaenda kituoni kudai baiskeli yake.
Pale kituoni Mkuu wa kituo alimuita askari aliemkamata ili ampe baiskeli yake, askari akakiri kumkamata yule kijana ila akamuomba mkuu wa kituo aongee na yule kijana pembeni. Askari akamlaumu yule kijana kwa nini anataka kumharibia kazi? Kijana nae akakomaa na kudai apewe baiskeli aliyokamatwa nayo. Huku na huku, ikabidi yule askari atafute pesa na kununua baiskeli mpya ya kumlipa yule kijana.
Yule kijana alipokabidhiwa baiskeli mpya akafungua taa na kumkabidhi askari. Akamwambia "baiskeli haikuwa na taa". Jitahidi kutenda haki bila kujali hali ya unaemtendea haki.