KERO Bajaji jijini Mwanza wanapaki hovyo sehemu ambazo si salama na usumbufu kwa watumiaji wengine wa barabara

KERO Bajaji jijini Mwanza wanapaki hovyo sehemu ambazo si salama na usumbufu kwa watumiaji wengine wa barabara

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Prince05

Member
Joined
Feb 27, 2024
Posts
43
Reaction score
84
Ukiwa KENYATA ROAD (Mataa/Makoroboi) hadi kufika nata bajaji zimekua nyingi sana wa mbaya zaidi wanavunja sana sheria.

Wanapaki wanavyojisikia, wanageuza katikati ya barabara kuna wakati unaweza kuta zinatembea Bajaj mbili lane moja wamejaa wao mmoja kushoto mwingine kulia na wanatembea mwendo mdogo kusababisha foleni, huwezi ku overtake njia yote (lane) wameitawala wao. Kwa kifupi Bajaji zimekua ni kero kubwa sana kwa

MWANZA MJINI KATI.

Wanatusaidia suala la usafiri lakini wengi wao hawajui matumizi ya barabara na sheria hawajui.

Suala la kupaki popote au double parking au twin parking ni hatari sana kiusalama na kusababisha kero kwa watumiaji wengine. Mamlaka zijaribu kuangalia suala hili.
1000178355.jpg
 

Attachments

  • PXL_20250320_135918852.jpg
    PXL_20250320_135918852.jpg
    718.1 KB · Views: 30
  • PXL_20250320_135911494.jpg
    PXL_20250320_135911494.jpg
    731.1 KB · Views: 31
Kama hawavunji Sheria na by laws za jiji la mwanza basi hawana makosa
 
Back
Top Bottom