Bajaji za Ferry-Kariakoo zifutwe

Bajaji za Ferry-Kariakoo zifutwe

crome20

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2010
Posts
1,193
Reaction score
810
Kama ni kukosa ubunifu basi ni kuendelea kuwa na bajaji za Ferry- K/Koo. Kwanza tuna usafiri wa uhakika wa Mabasi yaendayo kasi DART yanayofika sehemu zote za K/Koo. Kuna haja gani ya kuwa na utitiri wa bajaji zinazoongeza msongamano, vurugu, kelele katika barabara ya Samora na Uhuru?

Hizo bajaj zitafutiwe route nyingine pembeni ya mji ambako hakuna usafiri wa uhakika. Hii ni kuikosesha mapato huduma ya DART na kuchafua jiji. Kama kuna changamoto za kutumia mwendokasi zijadiliwe lakini suluhisho lisiwe kuwepo kwa hizo Bajaj.

Lakini pia ninashauri route ya daladala kutoka Makumbusho-Sinza-Posta zisipitie Shekilango- Morogoro Road, badala yake zipitie Kijiweni-kwa Mtogore-kutokea Magomeni.

Daladala hizi zimekuwa kikwazo kwenye barabara ya Morogoro sababu vituo vyake vilishafutwa na wanachofanya ni kupaki barabarani na kuongeza msongamano na usumbufu ikiwemo kusababisha ajali.

Kwa kufanya hivya tutaongeza ufanisi wa matumizi ya barabara. Wenye akili wataelewa. Asante.
 
Mjibu kwa hoja mkuu, kujibu tu eti "wivu tu" inaonekana hauna akili.

Inatakiwa umjibu kwa hoja ili tupime uzito wa hoja.
Ila kwa ulichojibu, akili hauna.
[emoji23][emoji23][emoji23] kwakweli mkuu
 
Kama ni kukosa ubunifu basi ni kuendelea kuwa na bajaji za Ferry- K/Koo. Kwanza tuna usafiri wa uhakika wa Mabasi yaendayo kasi DART yanayofika sehemu zote za K/Koo. Kuna haja gani ya kuwa na utitiri wa bajaji zinazoongeza msongamano, vurugu, kelele katika barabara ya Samora na Uhuru?

Hizo bajaj zitafutiwe route nyingine pembeni ya mji ambako hakuna usafiri wa uhakika. Hii ni kuikosesha mapato huduma ya DART na kuchafua jiji. Kama kuna changamoto za kutumia mwendokasi zijadiliwe lakini suluhisho lisiwe kuwepo kwa hizo Bajaj.

Lakini pia ninashauri route ya daladala kutoka Makumbusho-Sinza-Posta zisipitie Shekilango- Morogoro Road, badala yake zipitie Kijiweni-kwa Mtogore-kutokea Magomeni.

Daladala hizi zimekuwa kikwazo kwenye barabara ya Morogoro sababu vituo vyake vilishafutwa na wanachofanya ni kupaki barabarani na kuongeza msongamano na usumbufu ikiwemo kusababisha ajali.

Kwa kufanya hivya tutaongeza ufanisi wa matumizi ya barabara. Wenye akili wataelewa. Asante.
Wewe dereva wa tax a.k.a UBER
 
BRT ya kutoka mtaa wa Kongo hadi Ferry imeanza lini?
Kwani kutoka Congo kwenda Gerezani au Msimbazi B kuna umbali gani? Au unadhani daladala zinazoishia mnazi mmoja wote wanafanya kazi hapo mnazi. Acha kufikiria kizembe
 
Back
Top Bottom