Bajaji zilivyopandisha bei zao 500 ni Upigaji

OleWako

Member
Joined
Sep 7, 2021
Posts
25
Reaction score
73
Route nyingi huku Dar bajaji zimepandisha bei zao jero au hata zaidi.

Kwanza bajaji kupandisha bei kunaeleweka kutokana na kuongezeka kwa bei ya mafuta na ni sawa kabisa. Lakini kiasi walivyopandisha bei haiko sawa.

Tufanye tu mahesabu madogo ya mfano:

Kwa route ya Mwenge-Goba kwa kauli ya dereva mmoja wanajaza lita 1 baada ya kwenda mara 3. Yani kwenda, kurudi na kwenda tena.

Kwa hiyo route moja kwa bei ya mafuta mpya inawagharamia Tsh. 1,270, ongezeko la Tsh. 330. Sasa kwa kila njia wanapakia abiria wanne. Kwa hiyo mwisho wa siku ni kupanda kwa bei ya mafuta kunachangia ongezeko la gharama la Tsh. 85 kwa kila abiria..

Sasa kwanini wanapandisha mia tano mia tano? Gharama za maisha zinaongezeka na mnataka kutupiga tena?

Pandisheni mia mia basi halafu acheni ukorofi wakati wa kudai..
 
huku nilipo washakubali matokeo badala ya kupandisha 500, wamepandisha 200 mkuu ,
Hao ni wastaarabu tu wameangalia na hai ilivyo

Ila hawa wengine wanacheza na fursa na ukiwagomea wanasusa
 
Kuna sehemu walipandisha jero, kutoka 1500 hadi 2000, jana naona wamerudi kwenye "default mode" bila kutaka!!

Wananchi wapo radhi kutembea, panapofaa daladala wanapanda, hizo bajaj zitapata wapi abiria.
 
huku nilipo kuna daladala haziko mbali, hivyo bajaji mara nyingi wakitoa jeuri wananchi wanaacha bajaji wanasogea kwenye daladala --- yani ni kama iran na hormuz tu mkuu
Hapo sawa ,wenye vita wamalizane haraka maana hali si hali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…