Bajeti 2021/22: Wadau tunakataa kodi ya Majengo kulipwa kwa LUKU


Yes hapo compliance 100% na cost of collection ni zero. Kwa sababu the revenue is tapped at source.
Ni ubunifu wa hali ya juu kama road licence.
😁😀😄
 
TATIZO TUNAKUFA MOYO KUONA MATUMIZI YA HIZI KODI! MBAKA LEO HAMNA ALIYEPIGWA MVUA YA MIAKA KWA KOSA LA UHUJUMU UCHUMI! HALAFU MTU WA HALI YA CHINI UJE TU UMWAMBIE ETI NI RAHISI..! DAH🤨
 
Hili la kukata kodi ya nyumba kwenye luku ninaweza kuafikiana nao iwapo tuu. katika unit 28 ninazonunua kutoka katika sh. 10,000/= wafanye yao kama kwenye REA na EURA....mfano 1%...jengo, 2% REA n.k ila wasiguse kwenye Unit zangu. AU WASHUSHE KABISHA UUZAJI WA UNIT BADALA YA TSH. 350, WAUZE THS 300, ALAFU HIYO TSH 50 WAPELEKE KWENYE MAJENGO. Mwanzo mgumu wakituelimisha tutaelewa tuu. WATANZANIA NI WAPOLE SANA NENA WAUNGWA IWAPO UKIMUELEWESHA. USITUMIE NGUVU WALA UBABE
 
Maeneo ya vyuo vikuu wanafunzi wengi wanaishi nje ya chuo yaani wamepanga sasa hii Kodi itawahusu na wanafunzi pia ? Au mim sielewi ndugu zangu
 
au iwe hiv.kama kod laki mbili kwa mwez unampa mwwnye nyumba raki na themanain.180. ile 20 utaifidia kwenye property tax

Sent using Jamii Forums mobile app
Umefunga mjadala.Umeelezea vizuri,mbona ipo kodi ya zuio(with holding Tax,analipa mpangaji,wanakatiana na mwenye nyumba kwenye kodi,kwa zile nyumba zenye kodi kubwa.
 
Waziri wetu wa fedha na washauri wake wana akili ya kuandika majina yao kwenye mawe tu, au sijui wanaishi sayari gani kiasi kwamba wasijue matatizo ya kudai mtu akatwe kodi ya manunuzi kwenye manunuzi ya umeme.
 
Ni kama vile Motor Vehicle inavyokatwa kutoka kwa mnunua mafuta na siyo mmiliki wa gari...
 
Bandugu, mi nauliza kuhusu madeni ya miaka iliyopita, ndo tumesamehewa au?
 
Hii kodi maana yake ni kuwaangushia mzigo wapangaji. wenye nyumba siku zote watapandisha pango kufidia kodi hii
 
Naomba kujua, kwa hiyo wale wanaohangaika kwenda kulipa Kodi za jengo jawajaelewa au Kuna lugha gongana hapa??
 
Kodi ya majengo kulipwa kwa luku
Kwangu mm ipo poa kabisa
12,000 kwa mwaka nimekubali bila shida yeyote
Maswali. ,
Risiti za malipo tutazipata wapi?
Nyumba yenye mita zaidi ya 2 hawa si watalipishwa mara 2 ufafanuzi hapa
Nimepanga kibanda cha biashara na kuna mita ya umeme hiki kibanda nauliza nacho ni jengo au jengo lina tafsiri gani?
Kodi ya jengo inalipwa kwa umeme luku je kodi ya ardhi italipwa kwa style gani ...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…