Haya maneno ni mazito sana na yanaonyesha hali halisi inayomkabili mtanzania wa kawaida. Assume mtu yuko kijijini ni Mkulima si wameisha sahau mafuta. Halafu huku Bongo viongozi wakiendeleza ufisadi? Nafikiri mwaka huu kama alivyosema PM Mawaziri wanaweza kupata kazi tena ya kuzomewa.
56. Mheshimiwa Spika, Inaeleweka kuwa sehemu kubwa ya mapato ya bidhaa zinazoagiziwa kutoka nje zinatokana na bidhaa za Petroli na Mafuta. Serikali imeweka viwango vya kodi katika mafuta vya juu hivyo kufanya gharama za usafiri wa abiria na bidhaa kuwa kubwa na kumuongezea mzigo Mtanzania anayeishi kijijini na kuyafanya maisha yake kuwa magumu zaidi. Kwa mfano kodi zote kwa jumla katika Petroli ni Tshs 545.10 kwa lita na kwa dizeli Tshs. 520.80 kwa lita. (Bei za mafuta ya dizeli kwa makao makuu ya mikao kwa tarehe 16-31 Mei 2008 ilikuwa kama ifuatavyo kwenye baadhi ya mikoa, Dar es salaam 1,654.09 petrol na 1,884.89 kwa dizeli kwa lita huku mafuta ya taa yakiwa 1,488.24 kwa lita, Kagera 1,748.93 petrol na 1,979.73 kwa dizeli kwa lita huku mafuta ya taa yakiwa 1,583.08 kwa lita, Kigoma 1,930 petrol na 2,080 dizeli kwa lita huku mafuta ya taa 1,550 kwa lita na hali katika mkoa wa Mbeya 1,850 petrol na 2,000 dizeli kwa lita huku mafuta ya taa 1,500 kwa lita) . kati ya wastani wa bei ya 1800/- kwa lita. Hizi ni bei za mijiji, vijijini ambako kuna umasikini uliokithiri na mahitaji ya nishati kwa ajili ya usafiri,kilimo n.k. wastani wa bei ni Tshs.2,200 kwa lita.