KakindoMaster
JF-Expert Member
- Dec 5, 2006
- 1,356
- 88
Bajeti ya wapinzania hata ya mwaka jana ilikuwa imesoma shule sana. Lakini kuna watu wanaendelea kuwaaminisha watanzania kwamba wapinzani bado hawawezi kutawala!
UFISADI MWINGINE SIJUI VIONGOZI WETU NI VIPOFU? AU NDIYO WANAONUFAIKA?
79. Mheshimiwa Spika, Taarifa mbalimbali za kitafiti zinaonesha kuwa Tanzania inapoteza mapato mengi sana katika madini ya vito kwa sababu ya uzembe na ufisadi. Kwa mfano, Katika soko la dunia mauzo ya Tanzanite mwaka 2005 yalikuwa na thamani ya Dola za kimarekani 400m. Hata hivyo rekodi ya Tanzania ni Dola 16m tu.Tuna taarifa kuwa Kenya ilipata tuzo kwa kusafirisha Tanzanite nyingi duniani wakati hawana Tanzanite.
Sisi ni Wajinga. Kama balozi zetu zinaajiri Wakenya (Sweden, kama tulivyoambiwa na wana JF wa huko) tunategemea nini?
Mkuu Kasheshe
Kwa hiyo unataka kumaanisha kuwa walio tengeneza bajeti wa serikali mambo yanawapiga chenga?
Maana hao wachache wameonyesha mapungufu ya kutosha na pia kwa mtazamo wangu ni kama waandaaji wa serikali wamepelekwa shule.
Tutakaposikiliza upande wa pili tutajua ukweli!!! ... tatizo ni kwamba kwa kuwa tunaandika tu hapa!!! tukikosea sawa... tukiandika upuuzi sawa... ndio maana tunajiona sisi maprofessa wa bajeti ... wakati hakuna lolote!!!
Hakuna kazi rahisi huku duniani kama kukosea mwingine!!!